BUKOBA SPORTS

Monday, June 4, 2012

KLABU YA FENERBAHCE YATANGAZA KUMNASA STRAIKA WA LIVERPOOL "DIRK KUYT"

Fenerbahçe imetangaza kwenye Akaunti yao ya Twitter kumnasa Straika wa Liverpool Dirk Kuyt kwa ada ya zaidi ya Pauni Milioni 1 na atasaini Mkataba wa Miaka mitatu.
Habari hizi pia zimethibitishwa na Klabu ya Liverpool kwamba Mchezaji huyo atakamilisha uhamisho wake katika Siku chache zijazo.
Kuyt alitua Liverpool akitokea Feyernood Mwaka 2006 na kuichezea Mechi 285 na kufunga bao 71.
Hivi karibuni Kuyt aligoma kurudi Klabu yake ya zamani Feyenoord akidai kuwa kama angerudi huko ingebidi mapato yake yapungue kwa Asilimia 80.

No comments:

Post a Comment