BUKOBA SPORTS

Friday, July 13, 2012

MAN UNITED: BILA PAUNDI MILL 10 BERBATOV HATUMTOI...


Berbatov
Matatizo na mawazo yanazidi kumzonga mchezaji wa Man United, baada ya timu yake hiyo kuweka wazi ya kuwa Berbatov anauzwa lakini sio chini ya paundi mil 10 pungufu ya hapo hatoki.
Kutokana na swala hilo kunaweza kukamlazimu mchezaji huyo kumalizia mwaka wake wa maisho uliobakia katika mkataba wake na timu hiyo.
Mchezaji huyo ambaye aliambiwa na kocha wake Ferguson ya kuwa anaruhusiwa kuondoka klabuni kutokana na kutohitajika, swala hilo la kuondoka linakuwa gumu kwa kuwa hakuna timu ambayo mpaka imekuwa tayari kutoa fedha kiasi hicho kikubwa kwa mchezaji ambaye hahitajiki na sio hivyo tu bali ambaye ameweza cheza mechi tano (5) tu msimu uliopita.


WATATU WAJIANDAA KUONDOKA LIVERPOOL.
Wachezaji watatu ambao inasemekana kuna uwezekano mkubwa kuondoka Liverpool ni….
Maxi
Maxi Rodriguez anatarajiwa kurudi nyumbani kwao Argentina huku timu ya Newell’s ikijiandaa kumpokea mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa Liverpool anataka kusajiliwa na klabu ya Newell’s Old Boys ya nchini kwao Argentina.
Maxi mwenye umri wa miaka 31 amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake aliokuwa nao na Liverpool lakini mbali na hivyo Sekretari wa timu ya Newell’s Pablo Morosano alisema,
“Tunasubiria taarifa rasmi. Kuna maongezi yanafanyika na Liverpool lakini sie tayari tumeshakubaliana na mchezaji mwenyewe (Maxi)“.
Maxi ni mchezaji ambaye alinunuliwa na kocha Benitez kutokea Atletico Madrid lakini chini ya makocha Hodgson na Daldlish hakuna fanikiwa kupewa nafasi nyingi za kucheza ingawaje pindi alipoitwa alitupia magoli.
Maxi ameweza fanikiwa kufunga magoli 15 katika mechi 48 alizocheza za ligi ya Uingereza.


Bellamy.
Bellamy nae inasemekana anataka kurudi nyumbani kunako klabu ya Cardiff.
Bellamy inasemekana yuko mbioni kujiunga na klabu ya Cardiff City.
Bellamy ambaye anajiandaa kushiriki mashindano ya Olmpic na timu yake ya GB (Great Britain) inasemekana hahitajiki Liverpool na hayupo katika mipango ya Rodgers kutokana na kwamba Rodgers anataka zaidi vijana.


Carroll
Tayari Newcastle wameshatoa paundi mil 10 kwa ajili ya kumrudisha mchezaji wao wa zamani.
Panauwezekano mkubwa Liverpool wakakubali kupoteza karibia paundi mil 20 kama wakimuuza mchezaji huyo kwa ada ya paundi mill 10 hii ni kwa kulinganisha na paundi mill 35 amabzo liverpool walitoa kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo.
Lakini kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo nako kutapelekea bei ya mchezaji huyo kupanda kama huko atakapoenda atafanya vizuri.
West Ham na Fulham wote wanamtaka Carroll huku kocha wa West Ham akimtaka mchezaji huyo kwa mkopo na Fulham wao wakitaka kumnunua kabisa kwa kutoa paundi mil 8 pamoja na Clint Dempsey.


 JAN VERTONGHEN HATIMAYE ATUA TOTTENHAM..



Sigurdsson (kulia),AVB na Jan (kushoto)
Timu ya Tottenham wamefanikiwa kumsajili beki wa Ajax Jan kwa paundi mil 10.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ndiye aliyekuwa nahodha wa Ajax alikubaliana na Tottenham maswala ya mshahara wiki iliyopita na sasa amekamilisha uhamisho huo kabisa kwa kupita mpaka vipimo.

Tottenham walidhibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wao wa twitter kwa kusema,
“Tunafurahi kutangaza ya kuwa @Jan-Vertonghen amekamilisha uhamisho wake wa kutokea Ajax baada ya kupita vipimo.
Akiongea baada ya kukamilisha uhamisho huo Jan alisema,
“Ninafuraha sana kukamilisha uhamisho huu.
Umechukua mda mrefu lakini hatimaye mie ni mchezaji wa Tottenham sasa.
Nina miaka 25 na najihisi ninuwezo wa kutosha kucheza katika ligi hii ya Uingereza.
Mwanzo Redknapp ndio alikuwa akinihitaji lakini sasa ni AVB kwangu mie hilo halinipi shida maadamu nitacheza mpira hilo tu ndio la maana kwangu”
Usajili huo ni wa pili kufanyika baada ya usajili wa kwanza wa Sigurdsson kukamilishika kutokea timu ya Hoffeinheim. 

No comments:

Post a Comment