>>MARUDIANO Novemba 17 huko Tunis!
Mechi ya kwanza ya Fainali ya kutafuta
Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, kati ya Al Ahly ya Misri na
Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia imechezwa Jumapili ndani ya Borg
El Arab Stadium Mjini Alexandria, Misri mbele ya Mashabiki 15,000, na
Timu hizi kutoka sare ya Bao 1-1.
Esperance ndio walitangulia kufunga
katika Dakika ya 49 kwa bao la Walid Hicheri na Al Ahly kusawazisha
katika Dakika ya 88 mfungaji akiwa Al-Sayed Hamdy.
Timu hizi zitarudiana huko Tunis, Tunisia hapo Novemba 17.
Mshindi wa Fainali hii atatawazwa kuwa
Klabu Bingwa Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na pia
ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa
Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.
AFRICAN CONFEDERATION CUP 2012
NUSU FAINALI
Ijumaa Novemba 2
Al Hilal [Sudan] 2 Djoliba AC [Mali] 0
Jumapili Novemba 4
AC Leopards de Dolisie [Congo] 2 El Merreikh [Sudan] 1
Marudiano
Jumamosi Novemba 10
El Merreikh [Sudan] v AC Leopards de Dolisie [Congo]
Jumapili Novemba 11
Djoliba AC [Mali] v Al Hilal [Sudan]
______________________________________
CITY HAIKO TAYARI KUSHINDA CHAMPIONS LEAGUE.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amesema kuwa kikosi chake kilichosheheni nyota walionunuliwa kwa pesa nyingi bado hakipo tayari kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kauli yao imekuja kufuatia mchezo wao dhidi ya Ajax Amsterdam utakaopigwa baada leo ambapo watalazimika kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo.
Pamoja na kuwa na wachezaji walionunuliwa kwa pesa nyingi mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Uingereza wamekuwa wakisuasua barani Ulaya baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu walioyocheza na kujikuta wakishika mkia katika Kundi D ambalo pia lina timu za Real Madrid na Borrusia Dortmund. Akihojiwa mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya West Ham United ambao City ilitoka sare ya bila ya kufungana, Mancini amesema kuwa hadhani kama kikosi hicho kipo tayari kushinda taji la ligi ya mabingwa kwasasa. Meneja huyo aliendelea huku akiwatolea mfano Chelsea kwamba wamesubiri kwa kipindi cha miaka 10 ndio wakaja kunyakuwa taji hilo msimu uliopita hivyo hata kwa City haitakuwa kazi rahisi haswa ikizingatiwa kundi gumu walilopangwa msimu huu na msimu uliopita.
City ilianza michuano hiyo kwa kukubali kipigi cha mabao 3-2 kutoka kwa Madrid kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Dortmund na baadae kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ajax nchini Uholanzi.
_____________________________________
FERGUSON ATANIA KUPIGA PENATI MWENYEWE BAADA YA WACHEZAJI WAKE KUKOSA MARA KWA MARA.
MENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa utani amependekeza kuwa anaweza kupiga penati mwenyewe siku nyingine baada ya Wayne Rooney kukosa penati wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal Jumamosi. Mabao ya Robin van Persie na Patrice Evra yalitosha kuihakikishia United alama zote tatu na kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingerezakwa mara ya kwanza msimu huu lakini timu hiyo ingeweza kupata mabao zaidi kama Rooney asingekosa penati baada ya Santi Cazorla kuunawa mpira katika eneo la hatari. Rooney anakuwa mchezaji wa`nne wa timu hiyo kukosa penati katika michezo ya hivi karibuni baada ya Van Persie, Javier Hernandez na Nani na kukosa nafasi kama hiyo msimu huu.
Ferguson amesema kuwa amsikitishwa na kitendo cha Rooney kukosa penati hiyo lakini suala la msingi lilikuwa ni ushindi kwenye mchezo huo hivyo anashukuru walifanikiwa huku akitania kuwa kama itatokea nafasi nyingine ya kupiga penati katika mchezo mwingine atapiga mwenyewe..
Rooney akichonga penati...
No comments:
Post a Comment