BUKOBA SPORTS

Monday, November 5, 2012

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: SCHALKE VS ARSENAL, MANCHESTER CITY VS AJAX - TIMU 16 DIMBANI LEO, MANCINI ASUBILIA MIUJIZA LEO USIKU!!

Mechi za UEFA Raundi ya nne zinaendelea kutimua vumbi leo hii Jumanne Usiku na Siku hii Timu mbili za England, Arsenal na Man City, zipo Uwanjani huku Arsenal wakiwa ugenini kucheza na Timu ya Ujerumani, FC Schalke, ambayo katika Mechi iliyopita huko Emirates, iliichapa Arsenal 2-0 na huko Uwanja wa Etihad, Mabingwa wa England, Man City, wapo nyumbani kurudiana na Ajax Amsterdam ambayo waliifumua City 3-1 katika Mechi iliyopita.

RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv v FC Porto
Paris SaintvGermain FC v GNK Dinamo
FC Schalke 04 v Arsenal FC
Olympiacos FC v Montpellier Hérault SC
RSC Anderlecht v FC Zenit St. Petersburg
AC Milan v Málaga CF
Manchester City FC v AFC Ajax
Real Madrid CF v Borussia Dortmund


KUNDI B
FC Schalke 04 v Arsenal FC
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Schalke Pointi 7
2 Arsenal 6
3 Olympiacos 3
4 Montpellier 1


Schalke 04 wanawania kuchukua mwanya wa kulegalega kwa Arsenal hivi karibuni na kupata ushindi wao wa pili dhidi yao watakaporudiana huko Ujerumani Jumanne Usiku.
Wiki mbili zilizopita, Schalke waliinyuka Arsenal 2-0 Uwanjani Emirates kwa Mabao ya Kipindi cha Pili ya Wachezaji wa Holland, Klaas-Jan Huntelaar na Ibrahim Afellay.
Lakini zote, Schalke na Arsenal, Jumapili zilifungwa katika Ligi zao kwa Schalke kupigwa na Timu goigoi Hoffenheim kwenye Bundesliga na Arsenal kuchapwa 2-1 na Man United kwenye Ligi Kuu England.
Nahodha wa Shalke, Benedikt Hoewedes, amesema Kikosi chao kitakuwa na nguvu wakicheza Uwanja wa nyumbani na amehoji: “Tulishinda London, kwa nini tusishinde nyumbani Veltins-Arena?"
Tangu wafungwe nyumbani na Schalke, Arsenal wamekuwa wakisuasua na kupata ushindi mwembamba wa Bao 1-0 dhidi ya Timu ya mkiani QPR, kisha kuibuka toka kichapo cha 4-0 na kuitwanga Reading 7-5 katika CAPITAL ONE CUP na kuja kufungwa 2-1 Old Trafford na Man United kikiwa ni kipigo cha 3 katika Mechi zao 5 za mwisho.
Kwenye Mechi hii na Schalke Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, atamkosa Gervinho ambae atakuwa nje kwa Wiki 3 na pia majeruhi wengine ambao wamepona lakini hawajawa fiti ni Kieran Gibbs, Kipa Wojciech Szczesny, Abou Diaby na Tomas Rosicky.
Inabidi  mcheze kwa nguvu zenu zote. kumbuka tuna majeruhi wengi..
Mzee Wenger.

KUNDI D

Manchester City FC v AFC Ajax
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Borussia Dortmund Pointi 7
2 Real Madrid 6
3 Ajax 3
4 Manchester City 1

Roberto Mancini ametaka Kikosi chake cha Manchester City kicheze kiume katika Mechi zao 3 za UEFA CHAMPIONZ LIGI walizobaki nazo ikiwa watataka kufuzu kutoka Kundi D ambako wako mkiani wakiwa na Pointi 1 tu baada ya Mechi 3 za kwanza.
Jumanne Usiku, Man City watakuwa nyumbani kurudiana na Ajax ambayo iliitwanga City 3-1 katika Mechi iliyopita Wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, Mancini amekiri wanahitaji miujiza ili kufuzu kutoka Kundi ambalo lilibatizwa ‘Kundi la Kifo’ na amesema: “Sidhani kama tuko tayari kutwaa Ubingwa wa Ulaya. Sisi ni Timu nzuri lakini hatuko tayari kama Timu nyingine. Pengine Chelsea walikuwa Timu nzuri Ulaya kwa Miaka 10 na wamechukua Ubingwa baada ya Miaka 10, pengine hawakustahili!”

RATIBA:KESHO
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
Jumatano Novemba 7
Juventus v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
CFR 1907 Cluj v Galatasaray A.S.
SC Braga v Manchester United FC

No comments:

Post a Comment