BUKOBA SPORTS

Sunday, May 4, 2014

CHELSEA 0 v NORWICH 0, FULL TIME...BLUES YABANWA!! NORWICH BADO WAPO WAPO KWENYE MATUMAINI YA KUTOSHUKA DARAJA.

Norwich bado wamejiweka hai kubakia Ligi Kuu England baada kutoka 0-0 na Chelsea Uwanjani Stamford Bridge na kuifanya Chelsea ishindwe kukaa kileleni na kuibakisha Nafasi ya 3 Pointi 1 nyuma ya Liverpool na Vinara Man City huku wao wakiwa wamecheza Mechi moja zaidi.

Ikiwa Jumatatu Usiku Liverpool watashinda Mechi yao ya Ugenini na Crystal Palace basi yale matumaini finyu ya Chelsea kutwaa Ubingwa Msimu huu ndio yatatokomea kabisa kwani Liverpool watakwenda Pointi 4 mbele ya Chelsea ambao hawawezi kuzifikia kwani wana Mechi 1 tu.

Hii Leo Chelsea walipata Nafasi kadhaa za kushinda moja ikianguka kwa Nahodha wao John Terry aliekosa kwa Kichwa na mbili kwa Andre Schurrle na David Luiz ambao walipiga Posti.

Lakini nao Norwich watajutia ‘kunyimwa Penati’ baada baada John Terry kumwangusha Martin Olsson.Chupuchupu!!! John Terry alifanya ndivyo sivyo hapa!!Steven akiendesha mbele ya mchezaji wa Chelsea SalahGary Cahill kwenye patashika dhidi ya Johan Elmander wa NorwichBalaa!! Branislav Ivanovic juu kwa juuJohn Terry na mwamuzi wakiteta jambo!John Terry na Branislav Ivanovic wakilalamika kwa mwamuziMtanange ulikuwa mkali sana kipindi cha pili kwani kila timu ilitaka kushinda!John Terry akiendesha! kuona kama ataisaidia timu yake!!0-0 mpaka sasa!!!Frank Lampard wa Chelsea akiwa na wanae Luna na Isla, Mtanange ulipoisha!
Mpaka dakika zinamalizika hakuna timu iliyoliona lango la mwenzie....sasa ubingwa kwa Chelsea ni Miujiza!!

No comments:

Post a Comment