Juve, chini ya Kocha Antonio Conte, walitwaa Ubingwa huo wa Serie A kwa Misimu miwili iliyopita, ile ya 2011/12 na 2012/13, na wamekuwa Kikosi cha kwanza cha Juve kutwaa Ubingwa mara 3 mfululizo tangu Miaka ya 1930.
Juve wametwaa Ubingwa Msimu huu wakiwa na Mechi 3 mkononi na moja ikiwa ile ya Wikiendi ijayo dhidi ya AS Roma ambayo sasa wataingia bila presha.
Kesho Usiku Juve watacheza Mechi yao ya Serie A na Atalanta wakiwa kwao Juventus Stadium ambako, bila shaka, sherehe zitatawala.
Hili ni Taji la 30 la Ubingwa wa Italy kwa Juve na hivyo wataruhusiwa kuvaa Nyota ya Tatu ya Dhahabu kwenye Jezi zao kuanzia sasa.
Hata hivyo, wenyewe Juve wanasisitiza wao wametwaa Mataji 32 wakigoma kutambua kuvuliwa Mataji yao ya Misimu ya 2004/05 na 2005/06 baada ya Klabu yao kukumbwa na kashfa ya Upangaji Matokeo na kuadhibiwa kwa kuvuliwa Mataji hayo.
Hii Leo, mara baada ya habari kuvuja Kambini kwa Juve kwamba AS Roma wamechapwa na hivyo wao ni Mabingwa vifijo na nderemo vilitawala.
No comments:
Post a Comment