KIUNGO wa England, Adam Lallana atasherekea kuitwa timu ya taifa itakayoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka nchini Brazil kwa kusaini mkataba katika klabu mpya ya Liverpool kwa dau la paundi milioni 20.
Mpango wa kocha wa Liverpool Brendan Rodger ni kuongeza nguvu katika kikosi chake chenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi kuu soka nchini England tangu mwaka 1990.
Lallana alisherekea sherehe yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 26 kwa kuchagua kujiunga na Rodgers aliyeleta mapinduzi makubwa Anfield licha ya kuwepo kwa ofa nyingine kutoka klabu tofauti.
Southampton wanaamini bei waliyotaja ni haki kwasababu mchezaji huyo amekulia katika akademi yao na wanatamani kukamilisha dili hilo kabla ya mchezaji huyo kujiunga na kikosi cha Hodgson kitakachoweka kambi nchini Ureno kuanzia mei 19.
No comments:
Post a Comment