Bao mbili za Mchezaji wa Kimataifa wa Italy, Lorenzo Insigne, ziliifanya Napoli iende Mapumziko ikiwa Bao 2-1 mbele huku Bao la Fiorentina likifungwa na Juan Manuel Vargas.
Dries Mertens aliifungia Napoli Bao la 3 katika Dakika za Majeruhi.
Napoli walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Mchezaji wao Gokhan Inler kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 79 baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.
Mechi hii ilikuwa hatarini kufutwa kufuatia Mashabiki Watatu kupigwa risasi kutokana na vurugu za Mashabiki.
Kocha wa Napoli, Rafa Benítez, aliongea baada ya Mechi: “Ilikuwa Mechi safi. Tulianza vyema lakini walipopata Bao lao na sisi kuwa Mtu 10 ilibidi tujikaze tushinde.”
Hii ni mara ya 5 kwa Napoli kutwaa Coppa Italia na mara ya mwisho ni Mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment