Remy, ambae Msimu uliokwisha alichezea Newcastle kwa Mkopo kutoka QPR, alikuwemo kwenye Kikosi cha France kilichocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kilichotolewa Robo Fainali na yeye kuingia kutoka Benchi katika Mechi mbili dhidi ya Ecuador na Germany.
Jumatatu iliyopita Remy alikwenda huko USA ambako Liverpool wako kwenye Kambi ya Mazoezi na pia kushiriki Mashindano ya Guinness International Champions Club.
Liverpool imekataa kuzungumza lolote kuhusu kuvunjika kwa Dili hii.
Hadi sasa Liverpool imesaini Wachezaji Wanne kwa ajili ya Msimu mpya ambao ni Rickie Lambert, Adam Lallana, Emre Can na Lazar Markovic.
No comments:
Post a Comment