BUKOBA SPORTS

Sunday, July 27, 2014

USAJILI: ARSENAL YAMSAJILI KIPA WA COLOMBIA DAVID OSPINA

Arsenal wamefanikiwa kumsaini Kipa wa Colombia David Ospina kutoka Nice kwa Mkataba wa muda mrefu na kwa Dau ambalo halikutajwa.
Ospina, mwenye Miaka 25, amekuwa na Nice tangu 2008 na ameisaidia Colombia kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kufika Robo Fainali na kutolewa na Brazil.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “David ni Kipa mzuri. Ataongezea nguvu kwenye Kikosi chetu na tumefurahi sana.”
Tayari Wenger amedokeza Ospina anaweza kumpokonya Namba Kipa Namba Wani wa Arsenal Wojciech Szczesny.
Arsenal hivi karibuni walimsajili pia Alexis Sanchez

No comments:

Post a Comment