Taswira Viongozi na Timu zote mbili wakati wa dakika chache kumbuka Kiongozi wa mpira Aliyetangulia mbele ya haki kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Star Sylvester Marsh aliyefariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Mjini Mwanza.
Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika Mpambano huo wa Taifa Stars na Malawi CCM Kirumba Jijini Mwanza leo Jumapili tarehe 28.03.2015
Wimbo wa Taifa uliimbwa kabla ya Mechi kuanza, (Picha na Faustine Ruta)
Timu zote mbili kwenye mstari tayari kwa kuanza kipute
Kikosi cha Malawi baada Wimbo wao wa Taifa kumalizika kuimbwa
Kikosi cha Taifa Stars kikiimba wimbo wa Taifa
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza
Waamuzi wa Mtanage
Kikosi cha Malawi
Tayari kwa mpambano kuanza..
Shilingi kutafuta uelekeo
Mchezaji wa Malawi akimiliki mpira
Taifa Stars 0-1 Malawi dakika ya 3 mapema Malawi walishachafua ubao
Kipa wa Malawi akiondosha mpira langoni mwake
Pisha!
Fundi!
Kipa wa Malawi akiondosha mpira kwa kuupangua kutoka eneo la hatari
Mashabiki waliingia kwa wingi leo CCM Kirumba
Mashabiki jukwaa kuu
Meza Kuu Rais wa Tff Bw. Jamal Malinzi nae alikuwepo kushuhudia kipute!
Katikati ni Bw. Abdrazack kutoka Mjini Bukoba/Kasibante 88.5 FM Radio akitangaza live mpira huo kutoka CCM Kirumba Jijini Mwanza
Pambano hilo lililopigwa katika Jiji la Mwanza uwanja wa CCM Kirumba lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Stars wakitawala kwa kipindi kirefu bila ya mafanikio.
Goli la Malawi likifungwa dakika ya 3 na Esau Kanyenda mchezaji anayekipiga katika klabu ya Plolokwane City ya Afrika Kusini baada ya kipa wa Stars Mwadini Ali kushindwa kuudaka mpira wa kona huku Mabeki wakishindwa pia kumzuia mfungaji kupiga mpira ulioandika bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Licha ya kupiga mashuti 10 ambayo matano yalilenga goli Stars hawakufanikiwa kuongeza bao na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mpaka mapumziko Stars ilikuwa nyuma ya 1-0
Waamuzi wakitoka kwenda kupumzika wakati wa mapumziko dakika chache
Kipindi cha pili tunafanyaje??? Ngassa aingie au??
Muuaji wa bao la Malawi Essau kanyenda wakati wa mapumziko
Yale yale Ngassa na wenzake wakitoka Uwanjani kwenda kujumuika na kusikia neno kutoka kwa kocha mkuu Mart Nooij nini kinafanyika kipindi cha pili.
Patashika kwenye lango la Malawi kipindi cha pili. Hadi mapumziko Malawi walikuwa mbele kwa goli 1-0, na kupelekea Stars kurejea kipndi cha pili kwa nguvu, huku kukifanyika mabadiliko ya kumtoa Amri Kiemba na Haruna Chanongo na nafasi zao kuchukuliwa na Salum Aboubakari na Mrisho Ngassa.
Asante baba!! Samatta akipongezwa na Ulimwengu
Shabiki akifanya mbwembwe zake baada ya Taifa Stars kusawazisha bao
Samatta akipongezwa na Ulimwengu
Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars nao walimpongeza Samatta
Wakirudi kati kuanzisha mpira
Pongezi kwa Samatta Ally Mbwana
Wakishuhudia live Mtanange CCM Kirumba
Mtanange umemalizika dakika 90 kwa nguvu sawa 1-1
Waandishi wa Habari wakipata mahojiano moja kwa moja kutoka kwa Afisa habari wao Malawi akiwa sambamba na Baraka Kizuguto wa Tanzania kupitia Tff
No comments:
Post a Comment