BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 28, 2015

LEO LIVERPOOL UWANJANI KUCHEZA MCHEZO WAO WA KIPORO, STRAIKA DANIEL STURRIDGE NJE MPAKA MSIMU UJAO!

Liverpool wapo Nafasi ya 5 Pointi 7 nyuma ya Man United na Leo Jumatano wapo Ugenini kucheza na Hull City ambayo ipo hatarini kuporomoka Daraja.
Hii ni nafasi safi kwa Liverpool kuzoa Pointi ikiwa wataweza kuisambaratisha Timu inayoongozwa na Nahodha wa zamani wa Manchester United, Steve Bruce, ambayo nayo inapigania kubaki Ligi Kuu England.
Lakini Liverpool Jana walipata habari mbaya baada ya Meneja wao Brendan Rodgers kutoboa kuwa Straika wao mkubwa, Daniel Sturridge, huenda asicheze tena Msimu huu akiwa bado hajapona matatizo ya Nyonga na Paja lake.

Msimu huu, Sturridge amekuwa nje kwa kipindi kirefu na kurejea tena na Mechi yake ya mwisho kushiriki ni ile ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP walipoitoa Blackburn Rovers hapo Aprili 8.
Hull City wapo Nafasi ya 16, wakifungana kwa Pointi na Leicester City, wakiwa Pointi moja tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo ndizo hushushwa Daraja.

Kwa Liverpool, Mechi inayofuata kwao ni ya Nyumbani Anfield dhidi ya Timu nyingine inayosuasua mkiani, QPR, kisha Mechi zao zilizobaki Msimu huu ni dhidi ya Chelsea, Crystal Palace na Stoke City.
Ikiwa Liverpool watatetereka katika mbio za kufuzu 4 Bora na hivyo kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, Tottenham, waliofungana kwa Pointi na Liverpool na Southampton, walio Pointi 1 nyuma, bado wana matumaini ya kutinga 4 Bora. 


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumanne Aprili 28

21:45 Hull City v Liverpool
Jumatano Aprili 29
21:45 Leicester v Chelsea
Jumamosi Mei 2
14:45 Leicester vs Newcastle
17:00 Aston Villa vs Everton
17:00 Liverpool vs QPR
17:00 Sunderland vs Southampton
17:00 Swansea vs Stoke
17:00 West Ham vs Burnley
19:30 Man United vs West Brom


Jumapili Mei 3
15:30 Chelsea vs Crystal Palace
18:00 Tottenham vs Man City
Jumatatu Mei 4
22:00 Hull vs Arsenal

No comments:

Post a Comment