BUKOBA SPORTS

Thursday, April 30, 2015

LIONEL MESSI ATARAJIA KUPATA MTOTO WA PILI

Gazeti la Argentina, Clarin limeripoti tetesi nzito kuwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wanatarajia kupata mtoto wa pili.
Clarin limesema kuwa Messi na Roccuzzo hawajathibitisha habari hizo, lakini haijawazuia kuchapishwa stori hiyo kwenye gazeti lao.
Ripoti hiyo inasema Roccuzzo ana ujauzito wa miezi mitatu na mtoto ni wa kiume na wapenzi hao wameamua kuwa mtoto wao ataitwa Benjamin Messi.

Jina la Benjamin limetokea kuwa maarufu kwa wanasoka wa Argentina ambapo mtoto wa Sergio Aguero na mjukuu wa Diego Maradona anaitwa jina lake.
Messi tayari ana mtoto wa kiume aliyezaliwa Novemba 2012, jina lake anaitwa Thiago.
Kama tetesi hizo ni kweli, kwahiyo mtoto wa Messi anaweza kuzaliwa kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu 2015.

No comments:

Post a Comment