BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 28, 2015

BAYERN MUNICH 1 vs 1 BORUSSIA DORTMUND(AET, 0-2 PENATI) MIKWAJU YA PENATI YAWAANGUSHA BAYERN, WATUPWA NJE!! KLOPP ASHANGILIA TIMU YAKE KUSHINDA NA KUTINGA FAINALI!

Robert Lewandowski dakika ya 29 kipindi cha kwanza anaziona nyavu na kufanya 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund1-0
Bayern Munich 1-1 Borussia Dortmund (AET, 0-2 pens): Jurgen Klopp celebrates victory in
Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 75 aliisawazishia bao na kufanya 1-1.
Ndani ya Allianz Arena Jijini Munich, Germany ni patashika Fainali ya Kombe la Germany, DFB-POKAL, kati ya Miamba ya Nchi hiyo Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, na Borussia Dortmund.
Mchezaji wa Bayern Munich Philipp Lahm chini akipiga penati ya kwanza ..
Borussia Dortmund wametinga Fainali ya Kombe la Germany, DFB-POKAL, baada ya kuwabwaga Mabingwa Watetezi Bayern Munich kwa Penati 2-0 kufuatia Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Gemu iliyochezwa Nyumbani kwa Bayern, ndani ya Allianz Arena. 
Kwenye Fainali, Borussia Dortmund, ambao mwishoni mwa Msimu wanamuaga Kocha wao Jurgen Klopp, watacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine inayochezwa Leo kati ya Timu ya Daraja la 3 Arminia Bielefeld na Klabu ya Bundesliga, VfL Wolfsburg.Katika Nusu Fainali hii, Bayern walitangulia kufunga Bao la Dakika ya 29 la Robert Lewandowski na Dortmund kurudisha Dakika ya 75 kwa Bao la Mchezaji kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.Katika Dakika za Nyongeza 30, Dortmund walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Kampl kupewa Kadi Nyekundu lakini mwisho Bao zilibaki 1-1.Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Bayern walikosa Penati zao zote 4 zilizopigwa na Xabi Alonso, Philipp Lahm, Mario Gotze na Kipa Manuel Neuer huku Dortmund wakifunga 2 kupitia Sebastian Kehl na Ilkay Gundogan.
Lahm akipagawa chini baada ya kuwakosakosa Dortmund

Mchezaji wa Borussia Dortmund  Gabonese  Pierre-Emerick Aubameyang  akishangilia baada ya kusawazisha bao kwa kufanya 1-1 dakika ya 75 kipindi cha pili.

Kipa wa Bayern  Manuel Neuer akiunyakia ndani ya lango lake na kuwa bao

 Jurgen Klopp akifurahi na mchezaji wa  Bayern Munich Arjen Robben

Klopp akitoa maelekezo Uwanjani huku akiwa sare ya 1-1

No comments:

Post a Comment