BUKOBA SPORTS

Friday, May 1, 2015

MASHABIKI: BRENDAN RODGERS AFUKUZWE

Baada ya Jumanne kupigwa Bao 1-0 na Hull City na kuwaacha Pointi 7 nyuma ya Manchester United walio Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, Washabiki wa Liverpool wameibuka na kutaka Meneja wao Brendan Rodgers afukuzwe.
Liverpool wameshinda Mechi 2 tu kati ya 7 zilizopita na kuwaacha Nafasi ya 5 kwenye Ligi ambayo ni nje ya kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao na pia walitupwa nje kwenye FA CUP baada ya kutolewa na Aston Villa katika Nusu Fainali.
Msimu uliopita Brendan Rodgers nusura awape Liverpool Taji la Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Miaka 25 lakini wakateleza Mechi za mwishoni na Manchester City kutwaa Ubingwa na wao kubaki Nafasi ya Pili.
Gazeti moja huko England liliendesha Kura ambayo Watu 4,000 walipiga na Asilimia 65 walitaka Brendan Rodgers afukuzwe.

No comments:

Post a Comment