BUKOBA SPORTS

Saturday, June 13, 2015

KLABU YA ARSENAL YAPEWA SIKU 13 TU KUJIBU MASHITAKA YA FA, KWA KUKIUKA TARATIBU ZA UHAMISHO WA BEKI CALUM CHAMBERS!

Arsenal wamepewa hadi Juni 26 kujibu Mashitaka ya FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka taratibu za Mawakala wa Wachezaji wakati wa Uhamisho wa Beki Calum Chambers.
Pamoja na Arsenal, pia Wakala Alan Middleton amejumuishwa kwenye Mashitaka hayo na kupewa hadi Juni 17 kuyajibu.
Chambers, mwenye Miaka 20, aljiunga na Arsenal kutoka Southampton Julai 2014 na Msimu uliopita aliichezea Arsenal Mechi 36 na kuisaidia kukamata nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment