Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameadhibiwa na FA, Chama cha Soka England, kutokana na kauli yake na kupigwa Faini na kufungiwa Mechi 1 lakini Kifungo hicho kinasimamishwa kuangalia mwenendo wake.
Adhabu hiyo ya Faini ya Pauni 50,000 pamoja na Kifungo inatokana na kumshambulia Refa Robert Madley hapo Oktoba 3 mara baada ya Chelsea kukung’utwa 3-1 na Southampton.
Mourinho alikasirishwa na Refa Madley kutowapa Penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa Timu yake.
Kauli hiyo iliwafanya FA wamfungulie Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinalenga kuonyesha Marefa wanapendelea.
Wakitoa Adhabu hiyo, FA wamesema Kifungo cha 1 kinasimamishwa kuangalia mwenendo wake hadi Tarehe 13 Oktoba 2016 ambapo anatakiwa asitoe kauli au tamko lolote kinyume na Sheria ya FA E3 na akivunja hilo basi Jopo Huru litachukua mkondo wake na Adhabu hiyo itarejeshwa.

No comments:
Post a Comment