Maelfu ya wapenzi wa burudani Jijini Mwanza jana wamefurahia tamasha la Mziki Mnene linaloandaliwa na EFM radio na ETV za Jijini Dar es salaa ambapo wasanii mbalimbali akiwemo Kala Jeremiah walipata shangwe kubwa kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Krumba.
Wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki zao ni TID, Snura, Young Killer, Baraka Da Prince, Shoro Mwamba pamoja na Msaga Sumu huku Stone Fire akiibuka mkali wa Singeli Michano Mwanza baada ya kuwabwaga washiriki zaidi ya 20.
Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika anasema tamasha hilo mbali ya kuwa ni sehemu ya shukurani kwa wasikilizaji wa redio hiyo pamoja na watazamaji wa TVE, pia limelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hususani wa Singeli.
Tayari limekwisha fanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mtwara na Mwanza na kwamba litaendelea katika mikoa mingine hivyo mashabiki wa burudani waendelee kufuatilia EFM Radio na TVE kwa taarifa mbalimbali ikiwemo tamasha la Mziki Mnene linalopewa nguvu na Biko pamoja na Cocacola.
No comments:
Post a Comment