

Na Ripota wa Mafoto Blog, Shinyanga
KAZI nzuri iliyofanywa na kiungo wa Yanga, Ibrahimu Ajib Migomba katika dakika ya 24 na 30 imetosha kuwavunja nguvu Stand United na kuwahakikishia ushindi mnono watetezi wa Ubingwa wa Ligi Kuu Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa kambaragemjini Shinyanga jioni ya leo.
Kwa ushindi huo wa Yanga wa mabao 4-0 unaamsha shambrashambra za mchezo wa watani wa Jadi Yanga na Simba unaotarajia kpigwa Okt 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, baada ya Simba jana kuibuka na ushindi kama huo dhidi ya Njombe Mji huku Yanga nao leo wakifanya hivyo dhidi ya Stand United.

Pius Buswita akishangilia bao lake.....

Katika mchezo wa leo Yanga walinekana kutulia zaidi huku wakicheza kama wenyeji wa uwanja na kushambulia kwa kasi muda wote jambo lililowafanya Stand kushindwa kujiamini na kufanya papara kila walipofika katika lango la wapinzani.
Ibrahim Hajib Migomba, alifungua pazia la mabao ya Yanga katika dakika ya 24 kwa mpira wa adhabu baada ya Geofrey Mwashiuya kuchezewa rafu nje kidogo ya 18 na dakika sita baadaye alifanya kazi nzuri kwa kumalizia pasi nzuri ya Obrey Chirwa aliyepambana na kuwatoka mabeki wawili wa Stand United na kisha kupiga Krosi fupi ya chini iliyomkuta Ajibu na kufunga bao la pili akiwa katikati ya mabeki wawili.


****************************************
Bao la tatu lilifungwa na Kiungo Kiungo Pius Buswita katika dakika ya 53 akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Geofrey Mwashiuya na bao la kufunga pazia la mabao lilifungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 69 akiitendea haki pasi nzuri ndefu ya Pius Buswita, ambapo amzidi mbio beki na kupishana na kipa wa Stand kisha kuukwamisha wavuni mpira huo.
Baada ya mchezo wa leo Yanga sasa inafikisha pointi 15 sawa na watani wao Simba baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa nyuma kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa na watani wao Simba SC ambao pia wana pointi 15 sawa na Mtibwa Sugar walio nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment