Kipa David de Gea ameibeba Manchester United kwa kuokoa mpira kiufundi katika mchezo Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 ulioishia kwa sare tasa dhidi ya Sevilla.
Kipa huyo raia wa Hispania aliokoa mpira hatari ya Joaquin Correa na Steven N'Zonzi kabla ya kuonyesha ubora wake kwa kuokoa kwa mkono mmoja mpira wa kichwa wa Luis Muriel.
Manchester United ambao hawakuonyesha ushindani wa kutosha walipoteza nafasi za kufunga kupitia kwa Romelu Lukaku pamoja na Marcus Rashford aliyepaisha mpira golini.
Kipa David de Gea akiokoa kiufundi mpira wa kichwa uliopigwa na Luis Muriel
Paul Pogba akinywa maji (kulia) ni Martial ambao wote walianzia benchi.
De Gea aliokoa michomo mingi langoni mwake
De Gea aliokoa Mipira kama miwili ambayo Mashabiki wa Sevilla walikuwa wakijua tayari wamepata bao.
No comments:
Post a Comment