DEL PIERO AAGWA RASMI!!
Mabingwa wa Italia Juventus wamevunja rekodi ya AC Milan ya kutofungwa katika Mechi 42 baada ya kumaliza Msimu wa Ligi wa Serie A Jumapili kwa kuichapa Atalanta bao 3-1.
Pia Mechi hiyo ilikuwa ndio ya mwisho kwa Nahodha wa Juve Alessandro Del Piero baada ya utumishi wa Miaka 19 na aliweza kufunga bao la pili .
Pia Mechi hiyo ilikuwa ndio ya mwisho kwa Nahodha wa Juve Alessandro Del Piero baada ya utumishi wa Miaka 19 na aliweza kufunga bao la pili .
Ushindi dhidi ya Atalanta ni Mechi yao ya 43 ya kutofungwa kwa Msimu huu katika Mashindano yote na ikiwa Wikiendi ijayo watakwepa kufungwa kwenye Fainali ya Coppa Italia dhidi ya Napoli wao wataweka rekodi ya kuwa Timu ya kwanza kutofungwa katika Mechi za Ligi na Vikombe kwa Msimu mzima.
Msimu huu Juventus hawakushiriki Mashindano yeyote ya Vilabu Barani Ulaya na hilo limewasaidia kudumisha rekodi ya kutokufungwa.
No comments:
Post a Comment