Tuesday, May 29, 2018

SIMBA YAKABIDHIWA MILIONI 100 NA SPORTPESA

MABINGWA wa Tanzania klabu ya Simba imekabidhiwa hundi ya Sh. Milioni 100 na kampuni ya SportPesa Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
SportPesa Tanzania, ambao pia ni wadhamini wa mahasimu wa Simba, Yanga na Singida United imetekeleza kipengele cha mkataba wao kinachosema timu itakayotwaa ubingwa wa Ligi Kuu itapewa kiasi hicho cha fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, Oysterbay, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa kampuni hiyo, Abbas Tarimba aliwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba kwa kutwaa ubingwa kwani wameitendea haki nembo ya SportPesa
“Awali ya yote niwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba kwani mmewapa heshima kubwa wana msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu, Simba imeitendea haki nembo yetu ya SportPesa na kampuni inaamini kuwa wadhamini wakuu imekuwa ni moja ya chachu iliyosababisha Simba kuchukua ubingwa huu,” alisema Tarimba
“Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba Mei mwaka jana kuwa tutatoa bonasi ya Sh Milioni 100 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itachukua ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo bila shaka timu ni Simba”, aliongeza Tarimba
Pia Tarimba amewataka viongozi kupeleke kikosi kamili kwenye michuano ya SportsPesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 3-10 nchini Kenya ili iweza kuwa bingwa na kurudi na kitita cha dola za Kimarekani 30,000 pamoja na kupata nafasi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton FC ya Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park.
Naye Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi Kajuna aliishukuru SportPesa kwa kuleta mabadiliko kwenye soka nchini ambapo wao wameyaona kwa upande wao.
“Niwashukuru SportPesa kwa kuleta mabadiliko ya soka nchini ambayo sisi Simba tumeyaona na tutaendelea kutoa ushrikiano katika miaka mingine minne iliyosalia kwenye mkataba wetu”, alisema Kajuna
Simba ni miongoni mwa timu nne kutoka Tanzania zitakazoshiriki michuano ya SportPesa Super Cup itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Juni 3-10 ambayo yatashirikisha timu nane
Timu nyingine ni Yanga, Singida United na JKU ya Zanzibar, kutoka Kenya ni timu za Gor Mahia, AFC Leopards, Kakamega Home Boys na Kariabangi Sharks za Kenya. Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo baada ya kuwafunga watani wao wao jadi, AFC Leopard katika fainali mwaka jana zilizofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SIMBA WALIVYOKABIDHIWA MWALI WAO

MABINGWA wapya wa Ligi Kuu Bara Simba,jana walikabidhiwa ubingwa wao na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuri katika uwanja wa Taifa Dar es saam.
Simba walitwaa ubingwa huo,licha ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa bao 1-0 mbele ya Magufuri,hivyo kuvunjia rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika Ligi hiyo.
Mshambuliaji Edward Christopher ndiye aliyefunga bao hilo wakati mpira ukielekea ukingoni kunako dakika ya 85,kabla ya Simba kupata penalti dakika ya 93 iliyopigwa na Emmanuel Okwi na Juma Kaseja kupangua.
Aidha,Mgeni rasmi wa mchezo huo,Rais Magufuri aliwapongeza Simba kwa kutwaa ubingwa huo na kuwasihi kuendelea kupambana ikibidi watwae ubingwa wa Afrika.
Akizungumza kabla ya kukabidhi ubingwa huo,alisema Mabingwa hao walistahili kuchukua ubingwa huo,kutokana na namna walivyopambana,lakini hakusita kuipongeza Kagera Sugar kwa kuonesha mchezo mzuri.
Magufuri aliipongeza Wizara husika na uwongozi wa TFF kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika kuhakikisha mpira wa Tanzania unakuwa kila siku.
Pia alizungumzia ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa katika Jiji la Dodoma,ambapo alisema Serikali ipo katika mchakato huo na kuongeza matukio ya ajabu kama kung’oa viti hayapaswi kujirudia tena.
Ameziomba Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanja na kuomba visimamiwe kwa ubora wa hali ya juu kuhakikisha havivamiwi na mtu yoyote.
Naye,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe, alisema uwanja wa Taifa ndiyo utakaotumika katika michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa miaka 17 itakayofanyika mwakani katika ardhi ya nyumbani. Alisema uwanja huo na ule wa uhuru,vinahitaji marekebisho ya hali ya juu ili kuviweka sawa kabla ya michuano hiyo kuanza mwezi Aprili 2019.

COASTAL UNION YAMTUNUKU TUZO WAZIRI UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akipokea tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake kwa kuipandisha timu ya Coastal Union kucheza Ligi kuu msimu ujao kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu hiyo Salimu Bawaziri mapema leo kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipofungua mashindano ya Ligi ya Banda Cup . Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akionyesha waandishi wa habari tuzo aliyokabidhiwa na klabu ya Coastal Union kwa kutoa mchango wake kuipandisha kucheza Ligi kuu msimu ujao kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (CCM) Azzah Hamadi Hilali Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)kushoto akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuisaidia timu hiyo kuweza kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao tuzo hiyo walikabidhiwa pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano January Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli(CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM),Asas ya Iringa na Mo Dewji.

Friday, May 18, 2018

TASWIRA MWANANA ZA BARABARA YA KARAGWE-KYAKA-MKOANI KAGERA


Muonekano wa eneo la Mlima Kishoju uliopo kwenye barabara Karagwe hadi Kyaka mkoani Kagera ambayo barabara hiyo ni sehemu ya barabara kuu ya Kyaka – Bugene – Kasulo yenye urefu wa kilometa 183.1 ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Burundi.
Picha Na-Faustine Ruta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliifungua barabara hiyo ya Lami tarehe 07 Novemba, 2017 yenye urefu wa kilometa 59.1 iliyogharimu Shilingi Bilioni 81.597 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania na imejengwa na kampuni ya CHICO ya China.Friday, May 4, 2018

Atletico Madrid 1-0 Arsenal (agg: 2-1): Diego Costa aipeleka Atletico madrid Fainali

Diego Costa aliifungia bao mapema kipindi cha kwanza  Atletico Madrid na kuhakikisha Timu hiyo inasonga mbele hatua ya Fainali na Itakutana na Timu ya Marseille.
Costa akishangilia bao lake usiku kwe Europa Ligi mchezo uliochezwa usiku
Wachezaji wa Arsenal wakiwa hoi baada ya kutandikwa bao 
Meneja wa Arsenal,  Arsene Wenger akiwa hana la kufanya akijionea Vijana wake wakinyolewa bao

 Atletico Madrid wakiwapungia mashabiki wao mikono baada ya kusonga mbele

Wachezaji wa Atletico kwenye chumba cha kubadirishia nguo wakifurahia ushindi kwenye picha ya pamoja.

Thursday, May 3, 2018

TUMBAKU MORO, UCHUKUZI SC ZANG'ARA MEI MOSI

Kikosi cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha wake Mkuu Zenno Mputa (kulia) na Mshauri wa timu Kennedy Mwaisabula (Mzazi), kinachoshiriki katika michuano ya Kombe la Mei Mosi inayofanyika katika viwanja mbalimbali mkoani Iringa. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Mshambuliaji Ramadhani Madebe (23 jezi nyekundu) wa Uchukuzi akiwa katika msitu wa wachezaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joseph Mlimi (2), Mohamed Koshuma (16) na Stephen Mgendi (12) katika mchezo wa michuano ya Mei Mosi uliofanyika kwenye jana uwanja wa Samora. Uchukuzi walishinda bao 1-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Kipa Stanley Mwalega (aliyesimama kushoto golini) wa Tanesco akijiandaa kudaka mpira uliopigwa na Emmanuel Kiwea (2) wa timu ya Tumbaku ya Morogoro wakati wakicheza mchezo wa mechi ya Kombe la Mei Mosi ulifanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Winga Salum Idd wa Tumbaku ya Morogoro (11) akikokota mpira kuelekea langoni mwa Tanesco wakati wa mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tumbaku walishinda mabao 2-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).

Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
TIMU za Tumbaku ya Morogoro na Uchukuzi zinaongoza katika mchezo wa soka kwa kushinda kwenye michezo yao ya michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali mkoani Iringa.

Tumbaku ipo katika kundi `A’ inaongoza kwa kuwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili ikifuatiwa na timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), RAS Iringa na Hifadhi ya Ngorongoro, ambazo zote hazina pointi.

Nayo Uchukuzi inaongoza kundi ‘B’ baada ya kushinda mchezo mmoja nakuwa na pointi tatu, wakifuatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Geita Gold Mine (GGM) na NAO wote hawajakusanya pointi yeyote.

Katika hatua nyingine timu ya Tumbaku jana iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuwafunga Tanesco magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora.

Washindi walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 22 kwa njia ya penati lililofungwa Kelvin Makamba, baada ya mshambuliaji wao Issa Simbaliawa kufanyiwa madhambi na mlinzi wa Tanesco.

Bao la pili lilipachikwa katika dakika ya 32 na Ramadhani Shegodo aliyepata krosi safi kutoka kwa Idd Likasi.

Timu za soka zimegawanywa katika makundi mawili, ambapo kila kundi litatoa timu mbili zilizoshika nafasi za juu, na zitacheza hatua ya nusu fainali na fainali.

Mbali na soka michuano hiyo inashirikisha michezo ya netiboli, kuvuta kamba, karata, draft na bao kwa wanawake na wanaume.

Kesho timu ya kamba wanawake ya Tanesco itaumana na NAO, huku katika soka RAS Iringa watacheza na Hifadhi ya Ngorongoro katika uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa, na timu ya Uchukuzi itakutana na Ngorongoro katika mchezo wa netiboli utakaofanyika Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) na timu ya kamba ya wanawake ya Uchukuzi itavutana na MUHAS.

Sunday, April 29, 2018

MANCHESTER UNITED 2-1 ARSENAL, FELLAINI AWANYOOSHA GUNNERS DAKIKA ZA MAJERUHI!! ARSENE WENGER AKUTANA NA FERG OLD TRAFFORD


Marouane Fellaini alitokea benchi kipindi cha pili na kuifungia bao la kichwa na la Ushindi dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Man United Old Trafford. Bao hilo lilifingwa dakika za maeruhi. Man United imeshinda bao 2-1.

Baadhi ya Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Henrikh Mkhitaryan (katikati baada ya kusawazisha kipindi cha pili) Henrikh Mkhitaryan alikuwa mchezaji wa zamani wa Man United. Paul Pogba akishangilia bao lake la kwanza kwa Man United dakika ya 16,  Alexis Sanchez akiwa nyuma yake

Arsene Wenger akipewa zawadi na  Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa bosi wa Man United kabla ya mchezo kuanza.
Wenger akisalimiana na Ferguson pamoja na meneja wa sasa Jose Mourinho.

Konstantinos Mavropanos na  Jesse Lingard
Lingard plays a pass as Reiss Nelson watches on during the opening stages of the Premier League clash at Old Trafford

United's Serbian midfielder Nemanja Matic plays a pass under pressure from Arsenal youngster Ainsley Maitland-Niles

Mkhitaryan na Sanchez


 Calum Chambers akishuhudia mpira ukizama nyavuni

Pogba akishangilia mbele ya Mashabiki Old Trafford mapema dakika ya 16 baada ya kuitangulizia bao Man United kwa kufanya 1-0


 David De Gea nae kashangilia bao hilo

Mkhitaryan akigombea mpira dhidi ya Ashley Young

Mourinho
Romelu Lukaku  aliumia na nafasi yake ilichukuliwa na  Marcus Rashford