Monday, September 16, 2013

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014: RATIBA YA MTOANO: GHANA v MISRI, IVORY COAST v SENEGAL, NIGERIA v ETHIOPIA.


NCHI 10 za Afrika ambazo zimetinga hatua ya mtoano ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani zimejua hatma yao katika ratiba iliyopangwa katika makao makuu ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF yaliyopo jiji Cairo, Misri.

Timu hizo ambazo ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Misri, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Senegal na Tunisia ndio zinatafuta nafasi tano za kwenda kushiriki michuano hiyo nchini Brazil. Katika ratiba hiyo Ivory Coast ambao wataanzia nyumbani watakwaana na Senegal, Ethiopia wataikaribisha Nigeria,

Tunisia ambao waliingia katika hatua hiyo kwa mlango wa pili wataanza na Cameroon nyumbani. Wengine ni Ghana watakaokwaana na Misri wakati Burkina Faso wenyewe wamepangwa kuchuana na Algeria. Mechi hizo za mtoano zitachezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Octoba 11 na 15 na zile za mkondo wa pili zitachezwa kati ya Novemba 15 na 19 mwaka huu. 
Ghana itamenyana na Misri katika mechi za kuamua nchi ya Afrika itakayowakilisha bara zima katika dimba la kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Misri kama nchi pakee ambayo imeshinda mechi zake zote za makundi za kufuzu kushiriki kombe la dunia, bila shaka imeitia hofu nchi zengine na bila shaka hakuna ambaye angependa kukukutana nao.

Hii ni kutokana na matokeo ya draw iliyofanywa ambapo mataifa ya kiafrika zitacheza kwenye michuano ya kutafuta mwakilishi wa bara la Afrika Brazil mwaka ujao.
Mabingwa wa Afrika Nigeria watachuana na Ethiopia wakati Ivory Coast wakitoana jasho na Senegal.
Tunisia, waliofuzu baada ya Cape Verde watachuana na Cameroon.
Burkina Faso, nao waliomaliza wa pili katika michuano ya taifa bingwa Afrika watatoana jasho na Algeria.
Mechi za awamu ya kwanza ya michuano hiyo, zitachezwa kati ya tarehe 11 na 15 Oktoba, huku mechi za marudio zikichezwa kati ya tarehe 15-19 Novemba.
Shirikisho la soka duniani, Fifa, limezitaka nchi hizo kuchagua tarehe za mechi, eneo wanalotaka kuchezea mechi yao ya kwanza ifikapo Ijumaa wiki hii.
Wakati Ghana wanahisi kutokuwa na bahati baada ya kuamuliwa kuwa watacheza na Misri, wanaweza kujipa moyo kwani waliwahi kuwashinda Misri kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Dubai mwezi Januari.
Na haijulikani ikiwa Misri watacheza mechi yao ya marudio mjini Cairo kwani mgogoro wa kisiasa unatokota nchini humo.

RATIBA:
Ivory Coast v Senegal
Ethiopia v Nigeria
Tunisia v Cameroon
Ghana v Egypt
Burkina Faso v Algeria
11-15 October 2013: 1st leg
15- 19 November 2013: 2nd leg
5 playoff series winners qualify for 2014 FIFA World CupNo comments:

Post a Comment