BUKOBA SPORTS

Tuesday, February 11, 2014

ASKOFU JACKSON JAMES KABUGA WA KANISA LA (TAG) AZIKWA LEO NYUMBANI KWAKE KAGONDO KAIFO-BUKOBA. MAMIA YA WAKAZI WA BUKOBA WAJITOKEZA KATIKA MAZISHI HAYO!

MAREHEMU JACKSON JAMES KABUGA.
Amefariki usiku wa kuamkia ijumaa iliyopita jijini Dar es salaam alipopelekwa baada ya kutokea hospitali ya Bugando Mwanza akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo.
Mazishi yake yamefanyika nyumbani kwake Kagondo Kaifo Manispaa ya Bukoba.
Askofu Jackson Kabuga Alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita jijini Dar es salaam.

Mapema, Kanisani Marehemu Askofu Jackson Kabuga aliombewa misa katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG) kabla ya kuelekea Nyumbani kwake Kagondo nje kidogo na Mji wa Bukoba.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akitoa salam zake za mwisho kwa Marehemu Askofu Jackson Kabuga aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita jijini Dar es salaam.
Mtoto wa Marehemu akichukua kumbukumbu ya mwisho ya Baba yake kwenye Jeneza.
Katikati ni Mama Mjane wa Mchungaji Askofu Jackson Kabuga.
Mke wa Marehemu Askofu Jackson Kabuga.

Viongozi mbalimbali walihudhuria leo Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Hamugembe Bukoba kutoa heshima zao za mwisho.
Msafara kuelekea Nyumbani kwake Kagondo
Taswira ya Msafara kuelekea nyumbani kwa marehemu Askofu Jackson Kabuga Aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita jijini Dar es salaam.



Umati wa watu waendesha pikipiki wakiendesha kuelekea Nyumbani kwa Marehemu Askofu Jackson Kabuga.
Ilichukua umbali kama wa Kilometa 4 kufika kwake
Mchungaji JACKSON KABUGA, alizaliwa mwaka 1954 huko Kigoma Tanzania,ameishi mkoani Kagera kikazi na ameacha mjane na watoto 7.





Tayari gari limefika Nyumbani kwa Marehemu Askofu Jackson Kabuga Aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita jijini Dar es salaam.
Jeneza likipelekwa sehemu maalum ambapo atazikwa kwa mapumziko yake


Mama mjane wa Marehemu Mchungaji Jackson J. Kabuga
Sala maalum ya kumwombea marehemu Mchungaji Jackson James Kabuga ilichukua nafasi
Jeneza likishushwa chini tayari kwa maziko

Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk. Barnabas Mtokambali akiongoza mazishi ya marehemu Jackson Kabuga leo Kagodo.
Mama wa Marehemu pamoja na Mkewe wakiweka udongo
Watoto wa Marehemu Mchungaji Jackson J. Kabuga wakishiriki kumzika baba yao
Mama akiweka Shada la maua
Mama mjane wa marehemu Jackson James Kabuga akiweka shada juu ya kaburi la mumewe






Baadhi ya watoto wa Marehemu Askofu Jackson James Kabuga
Watoto wa Marehemu Askofu Jackson James Kabuga wakisikiliza neno kutoka kwa familia

Taswira Nyumbani kwa Marehemu

No comments:

Post a Comment