BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 10, 2012

LIVE KWENYE MAZISHI YA KANUMBA KINONDONI MAKABURINI LEO. MATUKIO TOFAUTI TOFAUTI

TUTAKUKUMBUKA DAIMA!


JENEZA LENYE MWILI WA KANUMBA UKIINGIZWA KABURINI 

 Mwili wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba ukiwa katika sanduku wakati ukiagwa kwenye Viwanja vya Leaders' Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Ray wa kwanza kushoto, Richie wa kwanza kushoto na wa pili ni Cloud, wa tatu ni Steve Nyerere
Nargis Mohamed wa pili kushoto, Happiness Magesse wa pili kulia
Watoto walioibuliwa na Kanumba kupitia filamu zake
aliyenyoosha mkono juu ni mama Kanumba
katikati Wema Sepetu akipenya, kushoto kwake Aunt Ezekiel
Jeneza lililobeba mwili wa Kanumba
Makamu wa rais mwenye miwani akiwa Dk Nchimbi na Mama Salam Kikwete
katikati ni dada yake Kanumba, Sara akisaidiwa
Steve Nyerere na msalaba
Mwili wa marehemu ukiwasili

 Maelfu ya waombolezaji wakjiwa kwenye viwanja vya Leaders kuaga mwili wa marehemu Kanumba
 Baadhi ya ndugu wa marehemu
 Mama wa marehemu Kanumba akiwa kwenye Viwanja vya Leaders
 Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiingia kwenye viwanja vya Leaders kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kanumba
 Waombolezaji wakiwa wamepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili wa Kanumba
 Kutokana na wingi wa waombolezaji ilibidi wengine wapande kwenye miti kujaribu kuuona mwili wa Kanumba
Polisi wa farasi wakiimarisha ulinzi kwenye eneo la Leaders


 Kamanda Kova akiweka mambo sawa mara baada ya watu kuzidi kusogea sehemu ya kaburi,na kufanya shughuli ya mazishi kusimama kwa muda.. 
 Waziri Nchimbi akijadiliana jambo na baadhi ya wanakati ya mazishi ya marehemu Kanumba mchana huu.
 Mh. Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo pia yupo makaburini hapa kuhakikisha shughuli inakwenda sawa.
 Waombolezaji.
 ulinzi upo na ulikuwa ukijitahidi kwa kila hali kuwadhibiti watu wasisogee sehemu lilipo kaburi la Kanumba.
 kwakeli watu ni wengi sana makaburini hapa na kuna wengine ambao wanaanguka kwa kukosa hewa,ila vijana wa red cross wako makini katika hilo.
 Wanahabari nao wanapata picha kwa shida  sana maana watu ni wengi kupita kiasi makaburini hapa.
 Waombolezaji wengine wakiwasili makaburini hapo.
 Mama wa Marehemi Steven Kanumba akiwasili Makaburini hapa akiwa ameambatana na Dada Asha Baraka.
 Muda mfupi uliopita kuna watu ambao walikuwa juu ya mti namna hii na tawi la mti limekatika na kuna baadhi ya watu wameumia na kukimbizwa hospitali.na Kamanda Kova ametoa amri kwa watu wote walio juu ya Miti washuke mara moja maana wanaweza kupata madhara makubwa zaidi. 


Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
 Waombolezaji wakitayarisha jeneza la marehemu Steven Kanumba tayari kwa kuliweka kaburini.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa baada ya kupoteza fahamu makaburini.
 Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya Sementi kwa ajili ya kufukia.
 Maqma wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua mkaburini
 Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wamefanya kazi ya ziada kutoa huduma ya kwanza kwa waombolezaji
 Maskari wa kusimamia usalama wakiweka uzio kwa ajili ya kuhakikiosha usalama katika mazishi hayo.
 Polisi wakiweka ulizi wa kutosha katika mazishi hayo.
 Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waombolezaji makaburini Kinondoni.
 Umati huu wote uko makaburini na wengine kama unavyoona wamepanda kwenye miti ili mradi tu waone mazishi ya mpendwa wao Steven Kanumba.
Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.

 
Polisi wa usalama barabarani na kazi ya ziada.
 
Watu walivyofurika kwa wingi.
 
Wengine juu ya miti.
 
Wasanii mbalimbali waliubeba mwili wa marehemu kutoka kwenye gari kuelekea sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuagia.

Huu ni umati wa watu unao elekea makaburini
Gari lililo beba mwili wa marehemu Steven Kanumba likielekea makaburini. 

 
















 

 

WEMA SEPETU AKIKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUZIMIA MAKABURINI NA KABLA MWILI WA MAREHEMU KUFIKA











ZAIDI ya watu 200 waliishiwa nguvu na kuanguka wakati wa mazishi muigizaji maarufu Steven Kanumba, miongoni mwao wakiwamo wasanii wawili maarufu nchini, Jackline Wolper na Wema Sepetu.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Slaam jana, Mwenyekiti waTiba na Kamati ya Mzishi Dk. Nassoro Ally alisema kuanguka kwa watu hao kumetokana na mkusanyiko mkubwa wa watu ambao ameulinganisha na ule ulijitokeza wakati wa mazishi ya Julius Nyerere.


Alisema hata hivyo, baadhi ya watu hao walioanguka wengi wao walipatiwa huduma ya kwanza akiwamo Wolpper na watu wa Msalaba Mwekundu na kisha kuruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi za muigizaji huyo maarufu Afrika.


Dk. Ally alisema hali hiyo,imekuwa ikijitokeza katika mikusanyiko kama ile ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ya moyo pia, kukosa hewa ya kutosha na wengine kuanguka kutoka juu ya miti walikokuwa wamepanda kushuhudia tukio hilo..


Kwa upande wa muigizaji Wema Sepetu hali ilikuwa mbaya ukilinganisha na mwenzake Wolper kwani ilibidi akimbizwe katika hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.


Wema akiongea Tanzania Daima akiwa kitandani hospitalini hapo alisema alijisikia ghafla akiishiwa nguvu na kushindwa kujitambua na kujikuta akianguka na kupoteza fahamu.


Alisema hali hiyo imechangiwa na njaa kwani alifika katika maeneo hayo ya Leaders akiwa hajapata hata kifungua kinywa, joto kali huku akizunguukwa na watu wengi kila alipokuwa akikaa.


Awali msemaji wa Hospitali hiyo ya Mwananyamala Edward Bisekala alisema hali yake siyo mbaya kama mnavyomuona akiwa na drip ambapo hali hiyo imesababishwa pressure.


Hadi Tanzania Daima ikiondoka hospitalini hapo majira ya saa 8: 15 kulikuwa na watu wapatao wanne wakiwa wamewekewa drip ambapo pia hali zao hazikuwa mbaya.


Aidha, katika hatua nyingine baba mzazi wa muigizaji huyo, Meshak Charles alisema malengo ya mwanaye kisiasa ilikuwa agombee ubunge mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Kwa mujibu wa Redio Wapo Kanumba alimwambia baba ake nia yake hiyo ambapo alikubaliwa na kuambiawa kuwa hilo ni chaguo lake kwani ana haki ya kuamua anachokipenda.

Charles alisema mipango yake hiyo ilikuwa ikienda vizuri kwani wakazi baadhi ya vijana walikuwa wakimuunga mkono kutokana na nia yake hiyo.

watoa huduma ya kwanza wakitoa watu waliozimia na kuwapeleka katika sehemu kwa ajili ya kuwapa huduma
Baadhi ya watu waliozimia wakiwa kwenye banda la Red Cros wakipata huduma ya kwanza
Nape Nnauye, Katibu wa itikadi na uenezi CCM, akizungumza na waandishi wa habari
Wilsoni Mukama, Katibu mkuu wa CCM, akizungumza na waandishi wa habari

  Yaliyojiri katika viwanja vya Leaders wakati wa tukio kubwa la kuuaga mwili wa Mwigizaji marehemu Steven Kanumba kama picha hii ya kwanza inavyoonyesha Makamu wa Rais akimfariji mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa, wakati alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu mwigizaji huyo aliyefanya vizuri sana katika tasnia ya filamu nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
 Waigizaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo kwenye viwanja vya Leaders leo.
 Rais wa shirikisho la filamu Nchini Bw. Saimon Mwakifwamba akimfariji mmoja wa waombolezaji katika msiba huo.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa juu juu baada ya kuzirai katikamsiba huo.
 Huyu naye hakujiweza ilibidi asaidiwe na wafanyakazi wa Msalaba mwekundu.
 Huyu muombolezaji naye alidondoka baada ya kupoteza fahamu na kuzirai katika viwanja vya Leaders.
 Watoto waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya Marehemu Kanumba.
 Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.
 Viongozi mbalimbali wamehudhuria katika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe, Waziri wa Ardhi na Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azzan.
Mtangazaji wa Clods TV Regina Mwalekwa akiwajibika katika tukio hilo la kihistoria kwenye viwanja vya Leaders.
 UMATI WA WATU AMBAO WAMETOKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KUJA KUSHUHUDIA MAZISHI

 MOJA YA MAKUNDI YA WATU MBALI MBALI AMBAO WANANGOJA KUSHUHUDIA MAZISHI YA MAREHEMU KANUMBA 

 HAYA NI MAKUNDI YA WATU AMBAO WAPO MBALI KIDOGO NA ENEO LA MAKABURI KUTOKANA NA KUFURIKA ENEO HILO




 WATU WAKIWA WANAWASILI MAKABURINI

 ASKARI WA USALAMA WA BARA BARANI WAKIHAKIKISHA HALI NI NZURI ENEO HILO

 HII NI AMBULANCE AMBAYO IMEBEBA WATU WALIO ZIMIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI MUDA HUU


Hii ni barabara ya Kinondoni kuingia kwenye makaburi ya Kinondoni ilikuwa ni balaaaa yani dah, kule mbele ndio mwili wa marehemu Steven Kanumba ndio unakuja
                Hapa ni baada ya mwili kupelekwa makaburini kinondoni.

Hii ni wakati naingia makaburini, watu walikua wengi sana na inaaminika kwamba ni zaidi ya watu elfu arobaini waliohudhuria leo.

Wengine walikosa nafasi karibu na kaburi la Kanumba.

Maelfu ya watanzania waliotaka kuuona mwili wa Marehemu Kanumba, wote walikosa nafasi ya kuutazama ulipokua Leaders kwa sababu iliamuliwa familia ya Kanumba tu na viongozi wachache wa Serikali ndio wamuage.
              

Makaburini Kinondoni.

Wakati msiba ukiendelea, hili kundi la vijana lilikua linapita karibu na eneo la mazishi na kuimba "tulidhani shemeji, kumbe muuaji" likimshutumu mwigizaji Lulu ambae anahojiwa na polisi sasa hivi kwa kudaiwa kumsukuma Kanumba mpaka kuanguka.


Barabara ya Kinondoni kulikua na foleni mbili, ya watu na ya magari.





 


Kwa wingi wa watu ilibidi watu wapande juu ya miti lakini baadae waliamuriwa washuke chini na kamanda Kova

Hii ndio sehemu ambayo mwili wa marehemu Kanumba unatarajiwa kuwekwa




Hawa watoto wanaopita ndio watoto waliokuwa wakicheza movie na marehemu Kanumba enzi ya uhai wake

Mama yake Kanumba aliyenyoosha mkono juu kuwapungia watu waliokuja uwanjani







Huyu dada hapa mbele alikuwa akilia kwa uchungu sana hadi nilikuwa namuonea huruma

Hemed na Yusuph Mlela wakiingia


                 





Makamu wa rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali



Mke wa rais Mama Salma Kikwete







Ray akiwa aamini kama swaiba wake ndio anakwenda kwenye nyumba yake ya milele





Charlz Baba akiwa na wenzake kutoka Mashujaa Band, Charz ameniambia walikuwa wanatokea Morogoro so waliweza kuwahi makaburini

No comments:

Post a Comment