Mmoja wa waombolezaji akisidiwa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu mara baada ya kuzimia katika msiba huo mkubwa.
Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Kundi maalum lililoandaliwa kwa nyimbo za maombolezo likiimba nyimbo za maombolezo katika katika msiba huo.
Jeneza la mwili wa marehemu Kanumba likiwa limewekwa tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho
Ndugu wa karibu wakielekea sehemu waliyotengewa kukaa.
Askari wa kike wakiweka sawa utaratibu wa waombolezaji kupita katika eneo hilo ili kukaa.
Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Saimon Mwakifwamba akizungumza katika msiba huo kutoa salamu zao za rambirambi kwa marehemu Steven Kanumba
Mmoja wa waombolezaji akipitishwa juu juu kwenye vichwa vya waombolezaji ili kupata huduma ya kwanza baada ya kuzirai, katikati anayetazama mbele ni Mussa Kisoky Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya jijini Dar es salaam.
Mwigizaji Steven Jacob kushoto akizungumza jambo na mbunge wa Maswa Mashariki Mh. John Shibuda katikati.
Mr Mtitu kulia akijadili jambo na mmoja wa waombolezaji wa
Utaratibu unapangwa na wanakamati wa kamati ya mazishi
Gari lililobeba mwili wa marehemu Kanumba linaondoka Leaders kwenda Makaburi ya Kinondoni huku likiwa limezungukwa na waombolezaji.
Umati wa waombolezaji ukiondoka kuelekea makaburi ya Kinondoni.
![]() |
Kwaya maalum ikiimba nyimbo za maombolezao katika msimba huo kwenye viwanja vya Leaders |
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga salute mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa heshima kwa marehemu Steven Kanumba. - www.bukobasports.blogspot.com
mama mzazi wa Kanumba akiwapungia mkono mashabiki wa mwanae waliokuwa viwanja vya leaders wakiuaga mwili wa marehem
watoto wawili walikuwa aki act na marehem Kanumba wakiingia viwanjani
Mwili wa marehemu ukifikishwa viwanjani tayari kwa kumpa heshima ya mwisho

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwasili viwanjani hapa.


Viongozi mbali mbali wapo kwenye shughuli hii ya kumuaga marehemu Steveen Kanumba.


Mdogo wa Marehemu Kanumba akiwasili viwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment