Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akikumbatiana na Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba wakati alipofika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhani msiba huo,jioni ya leo.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Rehema Nchimbi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 9,2012 kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Aprili 10, 2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya waombolezaji wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba Sinza jijini Dar es salaam Aprili 9, 2012 kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu.Picha na Ofisi Ya Waziri Mkuu

BONGO CELEBRITIES WAKIWA MSIBANI NYUMBANI KWA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Irene Uwoya akisaini kitabu cha waombolezaji kwa simanzi.

Mh. January Makamba Mbunge wa jimbo la Bumbuli, akiwasili msibani kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu.

Diamond akifuta machozi

Irenu Uwoya akiwa na simanzi kubwa.

Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (mbele) akiwa na Patcho Mwamba (nyuma kushoto mwenye miwali), wakiwasili msibani.

Jack wa Chuzi akiwa na majonzi msibani hapo.
Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu akisini kitabu cha maombolezo, pembeni kulia ni msanii Nyoshi Elsadat
Mh. January Makamba akisaini kitabu cha maombolezo
Msanii Naseeb Abdul "Diamond" akisaini kitabu cha waombolezaji alipofika msibani, nyumbani kwa marehemu Steve Kanumba Vatican Sinza
Msanii Bob Junior nae akitia saini katika kitabu cha waombolezaji.
Wasanii MwanaFA na Ambwene Yesaya nao walifika kutoa poole zao.Picha zote na GPL
Daktari aeleza kilichomwua mwigizaji Steven Kanumba
Florence Majani na Suzzy Butondo
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.
Baba mzazi azungumza Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba. “Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?’ Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake.” alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… “Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki.”
Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. “Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam,” alisema.

No comments:
Post a Comment