BUKOBA SPORTS

Wednesday, June 27, 2012

EURO 2012-NUSU FAINALI: SPAIN V PORTUGAL - TATHMINI YA MECHI

UWANJA: Donbass Arena, Donetsk, Ukraine SAA: 3 Dak 45 Usiku The main man: Cristiano Ronaldo and Portugal train at the Donbass Arena ahead of the first semi-final of Euro 2012HABARI ZA WACHEZAJI 

Portugal itamkosa Straika wao Helder Postiga ambaye ana maumivu pajani na hivyo Kocha Paulo Bento atalazimika kumchezesha Fowadi wa Besiktas, Hugo Almeida, badala yake. Kocha wa Spain Vicente del Bosque amethibitisha Wachezaji wake wote 23 wako fiti na huenda akawaanzisha Fernando Torres na Pedro kwenye Mechi hii.
TATHMINI YA MECHI
Wenyewe Spain wamekiri Timu ya Portugal si Timu ya kumtegemea Mtu mmoja ingawa wamekiri Cristiano Ronaldo ndio tishio kubwa kwao.Portugal itamkosa Straika wao Helder Postiga ambaye ana maumivu pajani na hivyo Kocha Paulo Bento atalazimika kumchezesha Fowadi wa Besiktas, Hugo Almeida, badala yake.
Kwenye Mechi ya mwisho Spain na Portugal kukutana, Mwezi Novemba Mwaka 2010, Portugal iliwabamiza Spain bao 4-0 na Ronaldo hakuwemo katika wafungaji.
Lakini kwenye michuano hii Ronaldo ndie aliefunga bao zote zilizowafikisha kwenye hatua hii na kumfanya afungane juu kwenye Listi ya Wafungaji bora na Straika wa Germany, Mario Gomez, kwa wote kufunga Bao 3 kila mmoja.
Kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi lao, Ronaldo alipachika bao zote 2 Portugal walipoibwaga Holland 2-1 na kwenye Robo Fainali, Ronaldo alifunga bao moja na pekee lililowapa Portugal ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Czech Republic.
USO KWA USO
•Spain wameifunga Portugal mara mbili tu katika Miaka 54 (Wameshinda 2, Sare 6, Wamefungwa 4).
•Hii itakuwa mara ya 35 kwa Spain kukutana na Portugal.
•Katika mara hizo 35, Portugal hawakushinda katika Mechi 15 za kwanza na walishinda kwa mara ya kwanza Mwaka 1948. Spain wanaongoza kwa kushinda Mechi 16 na kufungwa 6.
•Cristiano Ronaldo amefunga jumla ya Bao 6 kwenye Mashindano ya EURO na anazidiwa tu na Alan Shearer, Bao 7, na Michel Platini, Bao 9, ambao ndio Wachezaji waliofunga Bao nyingi kwenye historia ya Mashindano haya.
VIKOSI VINATARAJIWA
SPAIN: Casillas, Arbeloa, Pique, Sergio Ramos, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Alonso, Silva, Fabregas, Iniesta.
Portugal: Patricio; Pereira, Pepe, Alves, Coentrao; Meireles, Veloso, Moutinho; Nani, Almeida, Ronaldo
Refa: Cuneyt Cakir wa Turkey

No comments:

Post a Comment