
Kwa taarifa zilizopatikana kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari, zinasema kuwa msanii aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu, mwigizaji mahiri Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Marehemu Sajuki alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuwa amedondoka jijini Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita.
-Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Enzi za uhai wake
Sajuki na Mkewe Wastara Walipo kuwa kwenye viwanja vya Leaders wakati anawashukuru Watanzania na wasanii wenzake.
No comments:
Post a Comment