BUKOBA SPORTS

Saturday, March 31, 2012

LIGI KUU EGLAND: MAN CITY  YAPONEA CHUPUCHUPU


Huko Etihad, leo Manchester City, Timu inayowakimbiza Mabingwa na vinara wa Ligi Kuu England Manchester United katika mbio za kutwaa Ubingwa Msimu huu, imejikuta ikinusurika kupewa mkong’oto Uwanjani kwao na Sunderland baada ya kutanguliwa bao 3-1 na kusawazisha Dakika za mwishoni na mechi kwisha bao 3-3.
 
 Balloteli na Dzeko wakishangilia baada ya kufunga goli


Matokeo haya yamewafanya Man United, waliocheza Mechi 30, wabaki uongozini wakiwa na Pointi 73 na Man City, waliocheza mechi moja zaidi, wawe na Pointi 71.



MATOKEO YA MECHI ZA LEO JUMAMOSI MACHI 31
                  
                  Aston Villa 2 vs Chelsea 4
      Everton 2 vs West Brom 0
    Fulham 2 vs  Norwich 1
    Man City 3 vs  Sunderland 3
      QPR 2 vs  Arsenal 1
Wigan 2 vs  Stoke 0
Wolves 2 vs  Bolton 3

No comments:

Post a Comment