BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 3, 2012

MANCINI AHOFIA MATUMAINI YA UBINGWA KUYEYUKA KABLA YA KUCHEZA NA ARSENAL

 
 Jumapili ijayo Manchester City watatua Uwanja wa Emirates kucheza na Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England lakini kabla hawajaingia Uwanjani huenda wakajikuta wako Pointi 8 nyuma ya Mabingwa na vinara wa Ligi Manchester United na hilo limemtia wasiwasi Meneja wao Roberto Mancini.


Man City, waliocheza Mechi 31, wapo Pointi mbili nyuma ya Man United waliocheza Mechi 30 na ambao Jumatatu Usiku wanacheza na Blackburn na Jumapili ijayo, Masaa kadhaa kabla Man City hawajacheza na Arsenal, Man United wataikaribisha QPR Uwanjani Old Trafford.
 
 Mancini hivi karibuni
Ikiwa Man United watashinda mechi zao hizi mbili watakuwa Pointi 8 mbele na Mancini ametamka: ‘Tukiwa Pointi 8 nyuma, basi tumekwisha!’
Hata hivyo, ingawa Man United wameshinda mfululizo mechi 8 za Ligi walizocheza mwisho, Mancini amedai kuwa Mabingwa hao leo watatoka sare na Blackburn.

No comments:

Post a Comment