BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 3, 2012

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA VS AC MILAN KURUDIANA LEO


             RATIBA:
ROBO FAINALI--Marudiano
[Mechi ni Saa 3 Dak 45 Usiku]

[Matokeo ya mechi za kwanza katika mabano]
Jumanne Aprili 3
Bayern Munich v Marseille [2-0]
FC Barcelona v AC Milan [0-0]

Barcelona leo Usiku wapo kwao Nou Camp kurudiana na AC Milan katika mechi ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Kocha wao Pep Guardiola ametoa tahadhari ya kujiandaa vyema kuikabili vyema AC Milan ambayo walitoka nayo 0-0 katika mechi ya kwanza huko San Siro.

Guardiola amesema: ‘Ninahisi Milan watafunga bao!’
Na ikiwa AC Milan watapata bao kwenye mechi hii itabidi Barca wapige bao mbili ili watetee vyema Taji lao.
Msimu huu, katika mechi za Kundi, Barca na AC Milan zilitoka droo ya bao 2-2 huku Thiago Silva akifunga bao la kichwa Dakika za mwishoni na ikiwa leo pia matokeo ni hayo Barca watatupwa nje kwa bao za ugenini.
Guardiola ameonya: ‘Itabidi tufanye bidii kutafuta njia bora ya kuwashambulia! Wana nguvu sana katika kaunta ataki. Inabidi tuwashambulie, tukitafuta nafasi nyingi za kufunga! Milan watafunga lakini kazi yetu ni kusaka mabao mengi, kumiliki sehemu muhimu, kutawala mpira na kucheza pasi nyingi.’
Lakini huenda Barcelona wakamkosa Kiungo wao mahiri Xavi ambae ana maumivu ya musuli za mguu na leo atapimwa kama ataweza kucheza au la.
Pia Barca watakuwa na kazi ya ziada ya kumdhibiti Sentafowadi wao wa zamani Zlatan Ibrahimovich mwenye usongo baada ya kuondoka Nou Camp akiwa na bifu kubwa na Guardiola.
Nahodha wa Barca, Carles Puyol, amesema: ‘Wakishambulia ni hatari, wana Ibra, Robinho na Pato! Ibra ni vigumu kumdhibiti kwani ana miguvu sana!’
Nae Guardiola amesema: ‘Mipira ya juu ni ya Ibrahimovic! Ni mrefu kupita sisi, ana nguvu kupita sisi! Na mpira ukiwa kwenye boksi yeye ni hatari!’
Tegemeo kubwa kwa Barca, kama kawaida, ni Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, lakini katika Masaa 9 aliyocheza mechi dhidi ya Timu za Italia, Messi amefunga bao moja tu, tena la penati.

RATIBA:
ROBO FAINALI--Marudiano
[Mechi ni Saa 3 Dak 45 Usiku]
[Matokeo ya mechi za kwanza katika mabano]
Jumatano Aprili 4
Real Madrid v APOEL Nicosia [3-0]
Chelsea v Benfica [1-0]
NUSU FAINALI
MECHI kuchezwa Aprili 17/18 na Aprili 24/25
Marseille/Bayern Munich v APOELNicosia/Real Madrid
Benfica/ Chelsea v AC Milan/FC Barcelona
FAINALI
MECHI Kuchezwa Mei 19 Allianz Arena, Munich

No comments:

Post a Comment