BUKOBA SPORTS

Sunday, February 1, 2015

AFCON 2015: WENYEJI EQUATORIAL GUINEA WATINGA NUSU FAINALI! WAILAZA TUNISIA BAO 2-1.

Wenyeji Equatorial Guinea wameshinda Mechi yao ya Robo Fainali za AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Tunisia Bao 2-1 kwenye Mechi iliyokwenda Dakika 120 za Mchezo huko Estadio de Bata Mjini Bata.
Tunisia walitangulia kufunga katika Dakika ya 70 kwa Bao la Ahmed Akaichi na Equatorial Guinea kusawazisha kwa Penati tata katika Dakika ya 90 iliyofungwa na Javier Balboa.

Zilipoongezwa Dakika za Nyongeza 30, alikuwa Javier Balboa tena aliefunga Bao la Pili na la ushindi kwa Equatorial Guinea katika Dakika ya 102.
Equatorial Guinea sasa wapo Nusu Fainali na watacheza na Mshindi kati ya Ghana na Guinea.


Mwamuzi Rajindraparsad Seechurn  alipewa msaada wa Askari kuondolewa Uwanjani dhidi ya Wachezaji wa Tunisia baada ya Mtanange kumalizika.

Rajindraparsad chini ya ulinzi mkali

Hatari tupu!!

Kocha wa Equatorial Guinea Esteban Becker nae aliweka nguvu

Aliyeshinikiza vurugu aliwekwa kati...

Mwisho wa Mechi ilikuwa balaa!!

Akiongelea...

Bilel Mohsni wa Tunisia na Igor Engonga wa Equatorial wakipandishiana...
Hii Leo, Robo Fainali zitakamilika kwa Ghana na Guinea kucheza huko Estadio de Mongomo Mjini Mongomo na kufuatiwa na Ivory Coast na Algeria huko Nuevo Estadio de Malabo Mjini Malabo.

Washindi wa Mechi hizo 4 watatinga Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment