BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 2, 2012

LIGI KUU ENGLAND: FULHAM YAIFUNGA LIVERPOOL GOLI 1-0 KWA MARA YA KWANZA KWENYE UWANJA WA ANFIELD, BAO LA KUJIFUNGA WAO.

Plenty to ponder: Dalglish watched his second-string side lost at home to Fulham
Dalglish .... Siamini macho yangu Fulham kunichapia nyumbani ....
Timu ya Fulham kwa mara ya kwanza ilipata ushindi katika uwanja wa Liverpool wa Anfield 
Net result: Skrtel's own goal was enough to seal the points for Fulham
 Skrtel alijifunga bao mwenyewe na kuwawezesha  Fulham kujipatia ushindi na kuondoa ndoto za Liver.

Bao la kujifunga mwenyewe la Martin Skrtel lilileta masikitiko mengi usiku wa Jumanne wakati walipoikaribisha Fulham katika uwanja wa Anfield, na kuwasaidia wageni kuandikisha historia, ikiwa ni mara yao ya kwanza kupata ushindi katika uwanja huo. 
Net result: Skrtel's own goal was enough to seal the points for Fulham
Lakini inaelekea meneja wa Liverpool, Kenny Dalglish, hakuwa na wasiwasi mno, kwani tangu mwanzo aliichezesha timu dhaifu, wachezaji wake mahiri akiwapumzisha na anakusudia kuwatumia kikamilifu katika pambano la fainali la Kombe la FA mwishoni mwa wiki. 
Kop that! Liverpool have squandered a whopping 30 points at Anfield so far this season
Liverpool wameambulia pointi 30 tu Anfield mpaka sasa ligi hii inayokaribia kuisha
Liverpool walipata nafasi za kusawazisha, lakini Mark Schwarzer hakuwa mbunifu katika kumalizia na kuelekeza mikwaju vyema.
Fulham pia walishindwa kujiongezea mabao, kwani Kerim Frei aligonga mwamba, na kipa wa Liverpool Doni pia aliweza kuiokoa timu yake kutoka kwa makombora zaidi ya Pavel Pogrebnyak na Clint Demsey. 

Voting with their feet: There were many empty seats around Anfield for the visit of the west Londoners
Nafasi nyingi zilikosa watu, viti vilibaki bila mashabiki Anfield(Liverpool wamepotea msimu huu)

Voting with their feet: There were many empty seats around Anfield for the visit of the west Londoners
                                               Historia yaendelea kujirudia ya Liverpool
Matokeo hayo yanamaanisha Fulham sasa ina pointi 49, sawa na Liverpool.
Liverpool imo katika nafasi ya nane, na msimu huu imeshinda mechi tano tu, kati ya 18, na sasa wameachwa nyuma kwa pointi tatu na Everton, ambao pia usiku wa Jumanne walikamilisha mechi yao kwa sare ya 1-1 dhidi ya Stoke City.
Bila shaka mechi hii itakumbukwa na mashabiki wengi wa Liverpool, na ambao watajiuliza timu yao imejiandaa vipi katika kupambana na Chelsea katika fainali ya Kombe la FA, Jumamosi, tarehe 5 Mei.

No comments:

Post a Comment