Wednesday, July 29, 2015

KAGAME CUP: AZAM FC 0 vs 0 YANGA(PENATI 5-3) AZAM FC HAO NUSU FAINALI, WASHINDA KWA MIKWAJU YA PENATI!

Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza golipa wao Aishi Manula baada ya kudaka penati iliyopigwa na Hajji Mwinyi na kuivusha timu yake hadi kwenye hatiua ya nusu fainali ya Kagame
Azam Fc wameshinda na kusonga hatua inayofuata na sasa kukutana uso kwa uso na KCCA ya Uganda.

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donard Ngoma akiichambua ngome ya Timu ya Azama, wakati wa Mchezo wao wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Kagame, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penati 5-4, baada ya kutoshana nguvu kwa dakika 90 za mchezo.

Mshambuliaji wa Timu ya Azam, John Bocco akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Yanga, wakati wa Mchezo wao wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Kagame, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penati 5-4, baada ya kutoshana nguvu kwa dakika 90 za mchezo.

Beki hodari wa Timu ya Azam, Pascal Wawa akiruka juu kuwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donard Ngoma.

Beki wa Yanga, Juma Abdul akichezewa rafu na Mchezaji wa Azam, Frank Domayo.

Beki wa Timu ya Azam, Pascal Wawa akiangalia wa kumpatia mpira mbele ya Mshambuliaji wa Yanga.



Mwamuzi wa Mchezo kati ya Azam na Yanga, Davies Omweno akimuonyesha kadi ya njano Mchezaji wa Timu ya Azam, Kheri Abdallah baada ya kufanya kosa.

Washabiki wa Yanga watafakati kichapo walichokipata.





Mmoja wa washabiki wa Yanga akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu, wakati wa mchezo huo.

Wapiga picha wa vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia mchezo huo.













No comments:

Post a Comment