Wednesday, July 29, 2015

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: CHELSEA 2 vs 2 BARCELONA(4-2) PENATI. BLUES WASHINDA KWA MIKWAJU YA PENATI!

Suarez akitawanya wachezaji wa Chelsea ili apite!
Chelsea walitangulia kupata bao kupitia kwa Eden Hazard dakika ya 10 na kipindi cha kwanza kumalizika wakiwa mbele ya bao hilo 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Spain Barcelona.Kipindi cha pili dakika ya 52 Barcelona walisawazisha bao hilo kupitia kwa Luis Suárezkwa kufanya 1-1. Sandro Ramírez dakika ya 66 aliwaweka mbele Barca kwa kuwafungia bao la pili kwa shuti kali lililomzidi ujanja kipa wa Chelsea ndani ya Uwanja wa FedExField Maryland USA.
Kipindi hicho hicho cha pili dakika za wishoni ya 85 Gary Cahill aliisawazishia bao kwa kichwa na kuumia baada ya kupanguliwa kukutana mkono wa kipa wa Barca Ter Stegen.
Dakika 90 zilikatika kwa sare ya 2-2 na kwenda hatua ya Matuta na Chelsea kushinda kwa mikwaju hiyo ya penati 4-2.

VIKOSI:
CHELSEA:
Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Kenedy, Oscar, Hazard, Diego Costa
BARCELONA: Ter Stegen, Rakitic, Sergio, Suarez, Bartra, Douglas, Munir, Sandro, Adriano, Mathieu, Gumbau

No comments:

Post a Comment