Pienaar, Miaka 30, ambaye ni Nahodha wa Bafana Bafana Timu ya Taifa ya Afrika ya Kusini, amesaini Mkataba wa Miaka minne na Everton Klabu ambayo amekuwepo hapo kwa mkopo toka Januari.
Pienaar alianza Mechi 5 tu za Ligi Kuu England akiwa na Tottenham na tangu arejee Everton kwa mkopo aliichezea Mechi 14.
Everton wamelazimika kuimarisha safu yao ya mashambulizi baada ya kumpoteza Veterani wao Tim Cahill ambae amehamia huko Marekani na kujiunga na Klabu ya New York Red Bulls hivi juzi.
Pienaara alijiunga kwa mara ya kwanza na Everton akitokea Klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund Mwaka 2007 na akadumu hapo Miaka mitatu na nusu na ndipo Januari 2011 akenda Tottenham.
No comments:
Post a Comment