Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003.
Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.
Askofu Kilaini akisaini kitabu cha maombolezo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo
“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.
“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.
Marehemu ameacha mjane, watoto 11 na wajukuu 16.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.
Askofu Kilaini akiingia ukumbini kutoa pole kwa ndugu na jamaa
mjane Mke wa Marehemu (kulia)
umati wa watu waliokuja kumzika Merehemu Ndugu Meja Gen. Anatory Kamanzi
Mkuu wa mkoa wa Kagera na yeye akitoa pole kwa wafiwa
Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe(kushoto)
mwili wa marehemu ukipelekwa kaburini
Wanajeshi wakitoa heshima kuuaga mwili
Mke wa marehemu akiweka shada la maua
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Benson Bana(kushoto) kulia ni Faustine Ruta wa Bukobasports.com na yeye alikuwepo kuuaga mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima
No comments:
Post a Comment