BUKOBA SPORTS

Monday, October 1, 2012

CHELSEA YAENDA SWEDEN KUSAKA USHINDI WA KWANZA CHAMPIONS LEAGUE.

  MABINGWA wa soka barani Ulaya Chelsea ya Uingereza imesafiri kuelekea nchini Sweden kuifuata timu ya Nordsjaelland katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Meneja wa Chelsea Roberto di Matteo aakuwa akisaka ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Juventus katika mchezo wa kwanza wa kundi E uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge wiki mbili zilizopita. Mbali na mchezo huo pia kutakuwepo na michezo mingine ambapo Juventus nao wataikaribisha Shaktar Donetsk, Spartak Moscow watakuwa wenyeji wa Celtic, Valencia watapambana na Lille huku Benfica wakiwakaribisha mabingwa wa zamani wa michuano hiyo Barcelona. Michezo mingine ya kesho Galatasaray itakuwa mwenyeji wa Braga, huku BATE wakiwakaribisha Bayern Munich wakati CFR Cluj nao watawakaribisha Manchester United. 


SCHOLES, GIGGS, CARRICK, VALENCIA WOTE NJE MAN UTD UEFA KESHO

Rooney akijifua na wenzake leo
BEKI wa Manchester United, Jonny Evans atasafiri na timu kwenda Romania kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya CFR Cluj lakini Michael Carrick, Antonio Valencia, Paul Scholes na Ryan Giggs wote watakosekana katika kikosi cha Mashetani Wekundu.

Evans amekuwa na shaka ya uzima wake katika kikosi cha Sir Alex Ferguson, baada ya kutoka akichechemea mwishoni mwa mechi waliyolala 3-2 dhidi ya Tottenham Jumamosi, lakini kocha huyo Mscotland baadaye alidai kwamba beki huyo wa kati raia wa Ireland Kaskazini alipatwa na ganzi ya mguuni.

Beki huyo alifanya mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington lakini Carrick na Valencia walikosa mazoezi hayo, huku Valencia akiwa pia alikosa mechi dhidi ya Spurs kutokana na majeraha ya 'enka'.

Viungo mavetarani Scholes na Giggs, hata hivyo, wanaonekana kupumzishwa licha ya Ferguson kusisitiza kwamba atachezesha kikosi chenye uzoefu.

Yosso Scott Wootton na Michael Keane walifanya mazoezi na kikosi cha kwanza leo, pamoja na beki mpya Alexander Buttner, lakini Nemanja Vidic, Chris Smalling na Phil Jones wanatarajiwa kukosekana kwa muda mrefu.

Ashley Young pia hakushiriki mazoezi ya leo lakini alijifua na makocha wa viungo mbali na wenzake wa kikosi baada ya kuumia mwishoni mwa Septemba.
Beki wa zamani wa Man United, Mikael Silvestre pia alikuwapo na akafanya mazoezi na kikosi hicho, wakati beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa akisaka klabu mpya baada ya
kumaliza mkataba wake na Werder Bremen. Silvestre (35) anafanya mazoezi na Mashetani Wekundu kwa ajili ya kujiweka fiti.

Kikosi cha Manchester United kilichosafiri kwenda kuwavaa CFR Cluj:
De Gea, Lindegaard, Buttner, Evans, Evra, Ferdinand, Michael Keane, Rafael, Wootton, Anderson, Cleverley, Fletcher, Lingard, Nani, Powell, Tunnicliffe, Hernandez, Kagawa, Rooney, Van Persie, Welbeck.


 RATIBA
KESHO, Jumanne
Kundi E

    Juventus         v Shakhtar Donetsk       (saa 3:45) usiku
    Nordsjaelland    v Chelsea                    (saa 3:45) usiku

Kundi F
    Valencia      v Lille                                 (saa 3:45) usiku
    BATE Borisov  v  Bayern Munich         (saa 3:45) usiku
   
Kundi G

    Benfica        v Barcelona                       (saa 3:45) usiku
    Spartak Moscow v Celtic                       (saa 1:00) usiku
   
Kundi H
    CFR Cluj       v Manchester United        (saa 3:45) usiku
    Galatasaray    v Braga                            (saa 3:45) usiku

--------------------------------------------------------------------------------

KESHOKUTWA, Jumatano
Kundi A
    Dynamo Kiev v Dinamo Zagreb              (saa 3:45) usiku
    Porto       v Paris St Germain                   (saa 3:45) usiku

Kundi B
    Schalke 04 v Montpellier HSC                (saa 3:45) usiku
    Arsenal    v Olympiakos Piraeus             (saa 3:45) usiku

Kundi C
    Anderlecht          v Malaga                       (saa 3:45) usiku
    Zenit St Petersburg v AC Milan               (saa 1:00) usiku

Kundi D
    Manchester City   v Borussia Dortmund  (saa 3:45) usiku 
    Ajax Amsterdam    v Real Madrid            (saa 3:45) usiku

No comments:

Post a Comment