>>ALICHEZA KOMBE LA DUNIA NA HOLLAND 1978!!
FAHAMU kwa undani WASIFU wake!!
Klabu
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Yanga, leo imethibitisha kumchukua
Kocha mpya kutoka Uholanzi, Ernstus Wilhelmus Johannes Brandts, kwa
Mkataba wa Mwaka mmoja na leo ameanza rasmi kuinoa Timu hiyo huku
akikabiliwa na mtihani wake mkubwa wa kwanza hapo Jumatano Usiku kwenye
BIGI MECHI na Watani wa Jadi Simba kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom
itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Brandts, ambae ni Beki wa zamani wa Timu
ya Taifa ya Holland, amechukuwa nafasi ya Tom Saintfiet ambae Mkataba
wake ulikatizwa baada ya kutoelewana na Uongozi wa Yanga.
Brandts, mwenye Miaka 56, ambae akiwa
Yanga atakuwa na Wasaidizi Fred Felix Minziro na Kocha wa Makipa Mfaume
Athumani, mara ya mwisho alikuwa Kocha wa APR ya Rwanda.
WASIFU WAKE
JINA: Ernstus Wilhelmus Johannes Brandts
KUZALIWA: 3 Februari 1956, Nieuw-Dijk, Gelderland
KLABU ALIZOCHEZEA
1974–1977 De Graafschap
1977–1986 PSV Eindhoven
1986–1989 Roda JC
1988–1989 MVV Maastricht
1989–1991 K.F.C. Germinal Beerschot
1991–1992 De Graafschap
TIMU YA TAIFA HOLLAND
1977–1985 Mechi 28 Magoli 5
TIMU MENEJA
1993–2002 PSV Eindhoven (Timu ya Vijana na pia kama Msaidizi)
2002–2004 RKSV Nuenen
2005–2006 FC Volendam
2006–2008 NAC Breda
2009 Rah Ahan
2010–2012 APR FC
KUMBUKUMBU YA KIHISTORIA: Katika
Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1978, Brandts aliweka historia ya
kuwa Mchezaji pekee aliefunga Mabao kwa Timu zote mbili katika Mechi
moja pale kwenye Mechi ya Raundi ya Pili Holland ilipocheza na Italy
alipojifunga mwenyewe katika Dakika ya 18 na katika Dakika ya 50
kuifungia Timu yake Holland bao la kusawazisha na hatimae Mechi hiyo
kwisha kwa ushindi wa Bao 2-1 kwa Holland huku bao la ushindi likifungwa
na Arie Haan.
Brandts alisema amefurahishwa na
kujiunga na Yanga ambayo ni Timu kubwa katika Afrika Mashariki ambayo
pia anaifahamu vizuri tu baada ya kuiona wakati akiwa Rwanda na APR.
Kuhusu Mechi ya Simba Jumatano, Kocha huyo amesema anaifahamu Simba baada ya kuiona kwenye michuano ya Kagame Cup.
Kocha huyo amesema lengo lake ni kutinga
Uwanjani hiyo Jumatano kusaka Pointi 3 ili kuiinua Yanga ipate kuongoza
Ligi na hatimae kuwa Bingwa.
No comments:
Post a Comment