
Ikiwa Arsenal watafungwa na Bayern basi wapo hatarini ya kutofuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL kwa mara ya kwanza katika Miaka 16.
Hii si Mechi rahisi kwa Arsenal kwani Bayern watatinga Jijini London Uwanjani Emirates wakiwa na wimbi la ushindi la Mechi 12 mfululizo.
Lakini hilo halimtishi Wenger ambae amesema: “Sasa tupo katika hali nzuri na mkazo kwetu ni Mechi hii ya Jumanne.”
Arsenal hivi sasa wapo kwenye wimbi zuri la ushindi kwenye Ligi Kuu England ambalo limewapaisha hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Man City.
Mara ya mwisho kwa Arsenal na Bayern kukutana kwenye UCL ni Mwaka Jana walipotoka 1-1 huko Allianz Arena Jijini Munich na Bayern kushinda 2-0 Uwanjani Emirates katika Mechi yao ya kwanza.
No comments:
Post a Comment