BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 8, 2012

LIGI KUU ENGLAND: LIVERPOOL V CHELSEA LEO HAPATOSHI, LIVERPOOL WATAWAWEZA CHELSEA?

Injury blow: Petr Cech will miss Chelsea's game with Liverpool
LONDON, England
SIKU tatu baada ya kukutana kwenye Uwanja wa Wembley katika fainali ya FA, Liverpool leo watakuwa wenyeji wa Chelsea nyumbani Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu.

Chelsea wakiwa na furaha ya ushindi na kuendeleza rekodi nzuri ya kocha wa muda Roberto Di Matteo naye kipa Petr Cech anaamini ushindi wa Jumamosi umewaweka kwenye mazingira mazuri zaidi kuelekea katika fainali ya Ligi ya Mabingwa.

"Wakati unapokuwa bingwa wa FA na unaelekea kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, inakuongezea kujiamini zaidi na hali ingekuwa tofauti zaidi kama tungekosa ubingwa hapa," alisema Cech. "Tuna wiki mbili za kujiandaa na tunayo nafasi nyingi yakufikia mafanikio kama haya tena.
 Fernando Torres
Mwaka jana kocha Kenny Dalglish alijiunga na Liverpool na wakati wa usajili alisajili wachezaji wazuri, ambapo mashabiki wa Liverpool walikuwa wana imani timu yao itakuwa kati ya timu zitakazofanya vizuri katika Ligi Kuu ya England.
Go fouth: Chelsea's John Terry, Frank Lampard and Ashley Cole will all feature at Anfield
Lakini katika hali ya kushangaza katika Ligi Kuu ya England msimu huu kocha Dalglish ameleta maswali mengi kuliko majibu yaliyokuwa yakitarajiwa huku ndoto za Liverpool kurudi Ligi ya Mabingwa zikiota mbawa wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Liverpool ilichapwa bao 1-0 na Fulham katika mechi ya Ligi Kuu ya England na hivyo kuwaudhi mashabiki wake, kabla ya kufungwa tena na Chelsea 2-1 kwenye Kombe la FA.

Ubingwa Ligi Kuu ya England ukionekana ndiyo ilikuwa muhimu kwa Liverpool, na kocha Dalglish anakiri hilo.

"Kila mashindano unayoingia unataka kufanya vizuri kadri uwezevyo, katika Ligi Kuu tunacheza mechi 38, ambapo mwishoni nafasi uliyoshika inaonyesha mafanikio uliyoyapata,"alisema Dalglish.

Dalglish alisema ubingwa wa Ligi Kuu ya England ni mzuri, kwa sababu timu zote zinazoshindana katika ligi hiyo zinakuwa na fedha, timu zinazoshika nafasi nne za juu zinapata zawadi na kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya."

Mechi ya leo ya Liverpool dhidi ya Chelsea ni mechi ya 34 kwa timu hizo kukutana tangu Chelsea ianze kumilikiwa mwaka 2003 na tajiri wa Russia, Roman Abramovich.

Mechi ya leo itakuwa na upinzani mkali kwa sababu Chelsea pia Jumatano iliyopita ilimepoteza mchezo wake wa Ligi Kuu baada ya kuchapwa 2-0 na Newcastle United na hivyo kupoteza matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya England.

Chelsea pia itacheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Mei 19 mjini Munich.

Liverpool itawakosa  Charlie Adam na Lucas Leiva wanaosumbuliwa na majeruhi ya goti. Chelsea uenda ikiwakosa Gary Cahill na David Luiz wanaosumbuliwa na matatizo ya misuri.

No comments:

Post a Comment