BUKOBA SPORTS

Saturday, May 5, 2012

LIGI KUU ENGLAND: NEWCASTLE VS MANCHESTER CITY KESHO JUMAPILI SAA 9:30

Desire: Roberto Mancini wants his players to win the title
Baada ya kuitungua Manchester United bao 1-0 Jumatatu iliyopita na wao kukaa kileleni wakiwa sawa kwa Pointi lakini wana ubora wa tofauti ya magoli, Manchester City Jumapili wapo ugenini Uwanjani Sport Direct Arena kucheza na Newcastle na Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Swansea City. Wayne's world: The athletic effort has been voted the best of last 20 yearsMbali ya vita hiyo kuwania Ubingwa, Newcastle wao wapo kwenye kinyang’anyiro cha kumaliza 4 bora ili kucheza Ulaya Msimu ujao na wapinzani wao kwenye hilo ni Arsenal, Tottenham na Chelsea.

Katika Mechi yao ya majuzi, Newcastle, wakicheza ugenini Stamford Bridge, waliichapa bao 2-0 Chelsea kwa bao safi sana za Papiss Cisse na bila shaka Wadau wa Man United watakuwa wakisali Straika huyu ang'are tena.

Kule mkiani, wakati Wolves tayari ameshaporomoka Daraja, bado zipo nafasi mbili za kuungana nao na Timu zilizo mashakani kuzichukua ni Blackburn, Wigan, Bolton, Aston Villa na QPR.

RATIBA:
Jumamosi Mei 5
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Norwich
Jumapili Mei 6
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Newcastle v Man City         
[Saa 10 Jioni]
Aston Villa v Tottenham                                     
Bolton v West Brom
Fulham v Sunderland
QPR v Stoke
Wolves v Everton
[Saa 12 Jioni]
Man United v Swansea
Jumatatu Mei 7
[Saa 4 Usiku]
Blackburn v Wigan
Jumanne Mei 8
[Saa 4 Usiku]
Liverpool v Chelsea

No comments:

Post a Comment