Kwenye Fainali ya Coppa Italia, Napoli jana wamewachapa bao 2-0 Mabingwa wa Italia Juventus ambao walikuwa hawajafungwa Msimu mzima.
Hii ni mara ya kwanza kwa Napoli kutwaa Taji lolote kwa Miaka 22 na Kombe lao la mwisho likiwa ni Ubingwa wa Serie A Mwaka 1990 wakati huo wakiwa na Supastaa wa Argentina Diego Armando Maradona.
Mara ya mwisho kwa Napoli kutwaa Coppa Italia ilikuwa Mwaka 1987.
Kipigo cha leo cha Juve, kwa bao za Edinson Cavani na Marek Hamsik, kimefuta rekodi ya Juventus ya kutofungwa Msimu huu baada ya kushinda Mechi 26 na sare 16 na pia kumuaga vibaya Nahodha wao Alessandro Del Piero ambae leo ndio alikuwa akiiga rasmi Juve baada ya utumishi wa Miaka 19.
Napoli midfielder Marek Hamsik akishangila goli la pili
No comments:
Post a Comment