Kipa wa Manchester United David De Gea ameitwa kwenye Timu ya Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, kwa ajili ya Mechi za kirafiki dhidi ya Serbia na Korea Kusini kabla hawajaanza
Mashindano ya kugombea Ubingwa wa Nchi za Ulaya, EURO 2012, hapo Juni 8.
Hii ni mara ya kwanza kwa De Gea kuitwa kuchezea Spain ingawa ndiye Kipa wa Kikosi chao cha Vijana wa Chini ya Miaka 21 ambao Mwaka jana walitwaa Ubingwa wa Ulaya.
Wachezaji wengine walioitwa na Kocha Vicente Del Bosque kwa mara ya kwanza ni Wachezaji wawili wa Atletico Madrid, Juanfran na Adrian Lopez, na wengine ni Isco wa Malaga, Javi Garcia wa Benfica na Benat Etxebarria wa Real Betis.
Kikosi hicho cha Wachezaji 21 hakina Wachezaji wa Barcelona na Athletic Bilbao ambao watakutana Fainali ya Copa del Rey hapo Mei 25.
Pia, Wachezaji wa Chelsea Fernando Torres and Juan Mata hawamo pengine kwa vile Timu yao inacheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Bayern Munich hapo Mei 19.
Spain watacheza na Serbia Mei 26 na Korea Kusini Mei 30 na Mechi hizi zitachezwa nje ya Spain, kisha Juni 3 watarudi Seville, Spain kucheza na China.
Kwenye EURO 2012, Spain wako Kundi moja na Italy, Ireland na Croatia na watacheza Mechi yao ya kwanza na Italy Juni 10.
Spain inategemewa kutangaza Kikosi chao cha mwisho cha Wachezaji 23 kitakachocheza EURO 2012 Mei 27.
Kikosi kamili kilichoitwa:
Casillas (Real Madrid), Reina (Liverpool), De Gea (Man United), Arbeloa (Real Madrid), Ramos (Real Madrid), Albiol (Real Madrid), Alba (Valencia), Monreal (Malaga), Torres (Atletico Madrid), Dominguez (Atletico Madrid), Alonso (Real Madrid), Cazorla (Malaga), Etxebarria (Real Betis), Isco (Malaga), Garcia (Benfica), Soriano (Villarreal), Silva (Man City), Navas (Sevilla), Negredo (Sevilla), Soldado (Valencia), Lopez (Atletico)
No comments:
Post a Comment