BEKI Victor Costa atatolewa kwa mkopo Coastal Union ya Tanga wakati Derrick Walullya na Gervais Kago wanatemwa moja kwa moja na nafasi zao zinachukuliwa na Mussa Mudde na Patrik Mbiyavanga kutoka Jamhuri ya Kidem okrasis ya Kongo (DRC). Habari kutoka Simba zinasema kwamba, klabu hiyo haitaacha wachezaji wengi kwani inaamini ina timu imara na inahitaji kuboresha tu kikosi kwenye kuongeza wachezaji kulingana na udhaifu ulioonekana kikosini.
Costa anatolewa kwa mkopo Costa ili akajaribu kupandisha tena kiwango chake, baada ya hivi sasa kuonekana ameshuka ile mbaya. Costa ndiye aliyefanya uzembe uliosababisha Simba kufungwa mabao mawili katika kipigo cha 3-0 dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili nchini Sudan katika Kombe la Shirikisho. Kwa kufungwa 3-0 ndani ya dakika 90, Simba ililingana kwa mabao na wenyeji wao hao, baada ya Wekundu wa Msimbazi kushinda 3-0 awali Dar es Salaam, hivyo mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti. Simba ilitolewa kwa penalti 9-8.
No comments:
Post a Comment