Chelsea imeibuka Klabu Bingwa ya Ulaya baada ya kuibwaga Bayern Munich Uwanja wa nyumbani kwao Allianz Arena kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Mikwaju ya Penati 4-3 hapo jana kufuatia Mechi hiyo kuwa sare 1-1 katika Dakika 90 na Dakika 30 za nyongeza kutozaa lolote.
Hata hivyo Bayern Munich watajililia wenyewe kwa kutotwaa Taji baada ya kutawala Mechi yote na kukosa nafasi nyingi za wazi ikiwemo penati ya Arjen Robben mwanzoni tu mwa muda wa nyongeza wa Dakika 30 ambayo iliokolewa na Kipa wa Chelsea Petr Cech.
Chelsea imeibuka Klabu Bingwa ya Ulaya baada ya kuibwaga Bayern Munich Uwanja wa nyumbani kwao Allianz Arena kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Mikwaju ya Penati 4-3 hapo jana kufuatia Mechi hiyo kuwa sare 1-1 katika Dakika 90 na Dakika 30 za nyongeza kutozaa lolote.
Bila shaka Chelsea watamkumubuka sana Straika Didier Drogba ambae alisawazisha bao Dakika ya 88 na kufunga Penati ya mwisho iliyowapa ushindi.
Chelsea walikabidhiwa Kombe lao ambalo Nahodha John Terry, aliekuwa kifungoni, na Nahodha wa Mechi hiyo, Frank Lampard walilipokea kwa pamoja na kuamsha shamrashamra kubwa na furaha isiyo kifani iliyowaacha Mashabiki wa nyumbani wa Bayern Munich wakiwa wameduwaa na kulikumbuka pigo walilopewa na Timu nyingine ya England, Manchester United, ambao waliwatandika bao 2-1 Dakika za majeruhi kwenye Fainali ya Mwaka 1999 huko Nou Camp, Barcelona.
John Terry na Frank Lampard
Mbali ya kubeba Kombe, Wadau wa Chelsea sasa watamtupia macho Mmiliki wa Klabu, Roman Abramovic, ili kujua nini hatima ya Meneja wa Muda Roberto Di Matteo na nini kitamkuta Didier Drogba, Mwenye Miaka, 34 kwani Mkataba wake ndio unamalizika.
Drogba hapa alisababisha penati na mkwaju huo ukadakwa!
... Didier Drogba akishangilia dakika ya 90 baada ya kutupia nyavuni
Lilikuwa bonge la fainali na timu hizo zilimenyana vikali.
... Didier Drogba akifunga akifunga goli la mwisho la penati na kuibuka washindi
David Luiz na Mario Gomez kazini
MASHABIKI WA CHELSEA
MASHABIKI WA BAYERN MUNICH
Mara tu baada ya bao hilo, Kocha wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo, alimuinua mshambuliaji Fernando Torres kwenda kuchukua nafasi ya Solomon Kalou, jambo ambalo liliongeza uhai wa safu ya ushambuliaji ya Blues. Alikuwa ni mshambuliaji ambaye anacheza mechi yake ya mwisho na jezi ya Chelsea, Didier Yves Drogba aliyeisawazishia bao timu yake dakika ya 88, kwa kichwa kikali akiunganisha kona iliyochongwa na Juan Mata.
Bao hilo liliwanyamazisha malefu ya mashabiki wa Bavarians walioamini Mueller kamaliza kazi na Kombe linabaki Munich- na tangu hapo timu hizo zilishambuliana kwa zamu hadi kipyenga cha kuhitimisha dakika 90 na mchezo kuhamia kwenye dakika 30 za nyogeza.
Katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza, Drogba alimkwatua kwa nyuma kwenye eneo la hatari Frank Ribery na refa akawapa penalti Bayern sambamba na kumpa kadi ya njano mshambuliaji wa Ivory Coast.
Cech ambaye kesho anasherehekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake, hakupangilia mbali mpira huo, ilikuwa jirani mno na yeye na akaugeukia haraka na kuuficha kwenye himaya yake.
Baada ya hapo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na kwa tahadhari mno na hadi dakika 15 za kwanza zinamalizika ubao wa matokeo ulibaki kusomeka 1-1.
Dakika ya 107, Daniel Van Buyten alipata nafasi nzuri akiwa anatazamana na kipa Cech, lakini shuti lake la chini lilikwenda nje sentimita chache upande wa kuliwa wa kipa huyo wa Chelsea. Huna sababu ya kutosema lilikuwa bao la wazi walikosa Bayern.
Dakika ya 111 tena Bayern walifanya shambulizi kali langoni mwa Chelsea, lakini Luiz akaokoa na kuna iliyokwenda kupigwa na Robben, lakini ikaondoshwa kwenye hatari.
Chelsea captain John Terry akifatilia kwa makini sana na huku akiangalia akiwa amesimama!
Roman Abramovich naye alikuwepo akiangalia kazi ya vijana wake wa Chelsea - Munich
VIKOSI
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Tymoschuk, Contento, Schweinsteiger, Kroos, Robben, Mueller, Ribery, Gomez.
Akiba: Butt, Van Buyten, Petersen, Olic, Rafinha, Usami, Pranjic.
======================================================
Chelsea: Cech, Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole, Kalou, Mikel, Lampard, Bertrand, Mata, Drogba
Chelsea: Cech, Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole, Kalou, Mikel, Lampard, Bertrand, Mata, Drogba
Akiba: Turnbull, Essien, Romeu, Torres, Malouda, Ferreira, Sturridge.
Refa: Pedro Proenca (Portugal)
=====================================================MIKWAJU YA PENATI:
Phillip Lahm (Bayern)=Afunga 1-0
Juan Mata (Chelsea)=Akosa 1-0
Mario Gomez (Bayern)=Afunga 2-0
David Luiz (Chelsea)=Afunga 2-1
Manuel Neuer (Bayern)=Afunga 3-1
Frank Lampard (Chelsea)=Afunga 3-2
Ivica Olic (Bayern)=Akosa 3-2
Ashley Cole (Chelsea)=Afunga 3-3
Bastian Schweinsteiger (Bayern)=Akosa 3-3
Didier Drogba (Chelsea)=Afunga 3-4
TIMU ZA ENGLAND ZILIZOWAHI KUWA BINGWA WA ULAYA:
Liverpool (Mara 5)
Manchester United (3)
Nottingham Forest (2)
Aston Villa (1)
Chelsea (1)
MATCH FACTS
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Boateng, Tymoschuk, Contento, Schweinsteiger, Kroos, Robben, Muller (Van Buyten 86), Ribery (Olic 97), Gomez. Subs not used: Butt, Petersen, Rafinha, Usami, Pranjic.
Booked: Schweinsteiger.
Scorer: Muller 83.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole, Kalou (Torres 84), Mikel, Lampard, Bertrand (Malouda 73), Mata, Drogba. Subs not used: Turnbull, Essien, Romeu, Ferreira, Sturridge.
Booked: Cole, Luiz, Drogba, Torres.
Scorer: Drogba 88.
Referee: Pedro Proenca (Portugal).
Booked: Schweinsteiger.
Scorer: Muller 83.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Luiz, Cahill, Cole, Kalou (Torres 84), Mikel, Lampard, Bertrand (Malouda 73), Mata, Drogba. Subs not used: Turnbull, Essien, Romeu, Ferreira, Sturridge.
Booked: Cole, Luiz, Drogba, Torres.
Scorer: Drogba 88.
Referee: Pedro Proenca (Portugal).
Attendance: 69,901.
No comments:
Post a Comment