BAYERN MUNICH v CHELSEA
Jumamosi Mei 19
Saa 3 Dak 45 Usiku
Uwanja: Fußball Arena München
REFA: Pedro Proença wa Portugal
Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2011/12 itachezwa kati ya Bayern Munich na Chelsea Jumamosi Mei 19 Uwanjani Allianz Arena, ambao kwa Mechi hii tu kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München.
Wakati Chelsea na Bayern Munich zilipotinga Nusu Fainali za michuano hii wengi walidhani hawawezi kufika Fainali hasa kwa vile Wapinzani wao kwenye Nusu Fainali hizo walikuwa Vigogo wa Spain, Klabu za Real Madrid na FC Barcelona ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi.
Bayern Munich iliwabwaga Real Madrid na Chelsea ikawatupa nje FC Barcelona.
ZIFUATAZO ni DONDOO KUHUSU FAINALI HII na UKWELI NA TAKWIMU KUHUSU FAINALI ZA UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu zianze.NJIA ILIYOWAFIKISHA FAINALI:
UWANJA:
Allianz Arena, ambao kwa Mechi hii tu kwa sababu za kiudhamini, utaitwa Fußball Arena München.Huu ni Uwanja wa nyumbani wa Timu za FC Bayern Munich na TSV 1860 Munchen na uliteuliwa na UEFA kuwa ndio utachezewa Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Mwaka 2011/12 Januari 2009.
Ujenzi wa Uwanja huu ulikamilika tarehe 30 Aprili 2005 na Mechi ya kwanza kuchezwa ilikuwa ni Agosti 5, 2005 kati ya Bayern Munich na VfL Borussia Monchengladbach ambayo Bayern walishinda bao 3-0 wakishuhudiwa na Watazamaji 60,000 waliojaza Viti vyote.
KOMBE:
Machi 1967, UEFA iliamua kuiruhusu Real madrid ilichukue moja kwa moja Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kulitwaa mara 6. Kombe jipya lina urefu wa Sentimita 62 na uzito wa Kilo 7.5 na limetengenezwa kwa Madini ya Fedha.
Siku hizi, kwa mujibu wa kanuni za UEFA, Timu inaruhusiwa kulichukua Kombe hilo moja kwa moja ikiwa tu imeshinda Ubingwa wa Ulaya kwa jumla ya mara 5 au kushinda mara Kombe hili 3 mfululizo.
Hadi leo, baada ya Miaka 50 ya Mashindano haya, ni Real Madrid CF, AFC Ajax, FC Bayern München, AC Milan na Liverpool FC pekee ambazo zimeweza kupewa Kombe hili moja kwa moja.
MPIRA:
Mpira utakaotumika kwenye Fainali hii wa Kampuni ya Adidas unaitwa ‘Finale Munich’.
Hata hivyo, Mpira huu umekuwa ukitumika kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wote huu.
BALOZI MAALUM WA FAINALI-Paul Breitner
Paul Breitner, Miaka 60, aliwahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya akiwa na Bayern Munich, kuifungua Ujerumani bao kwenye Fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa Mjini Munich na maishani mwake amekulia Kilomita 50 tu toka Uwanja wa Allianz Arena.
Yeye ndio Balozi Maalum wa Mechi hii ambae pia aliwahi kuichezea Real Madrid.
FAINALI-19
Ushindi - 14
Sare - 5
Magoli - 49
Mechi kwenda Dakika 30 za nyongeza - 5
Mechi kumalizwa kwa Mikwaju ya Penati - 5
Matokeo ya kawaida = Bao 2-1 [Mara 4]
Timu zote mbili kufunga Mabao - Mara 10
Timu moja kufunga Mabao - Mara 8
Sare 0-0 = Mara 1
Jumla ya Dakika zilizochezwa Fainali zote = 1860
Kadi Nyekundu = 2
USHINDI MKUBWA
4-0 AC MILAN v FC Barcelona (Athens) 1994
3-0 REAL MADRID CF v Valencia CF (Paris) 2000
3-0 FC PORTO v AS Monaco FC (Gelsenkirchen) 2004
3-1 BV BORUSSIA DORTMUND v Juventus (Munich) 1997
3-1 FC BARCELONA v Manchester United FC (Wembley) 2011
USHINDI MKUBWA HAFTAIMU
3-0 AC MILAN v Liverpool FC (Istanbul) 2005
2-0 AC MILAN v FC Barcelona (Athens) 1994
2-0 BV BORUSSIA DORTMUND v Juventus (Munich) 1997
FAINALI ZILIZOAMULIWA KWA PENATI
1996 JUVENTUS waliitoa AFC Ajax 4-2 baada ya sare 1-1
2001 FC BAYERN MÜNCHEN waliitoa Valencia CF 5-4 baada ya sare 1-1
2003 AC MILAN waliifunga Juventus 3-2, sare 0-0
2005 LIVERPOOL FC waliibwaga AC Milan 3-2, sare 3-3
2008 MANCHESTER UNITED FC waliitoa Chelsea FC 6-5, sare 1-1
GOLI NYINGI KUFUNGWA NA MCHEZAJI MBILI
Daniele MASSARO AC MILAN 4 FC Barcelona 0 1994
Karlheinz RIEDLE BV BORUSSIA DORTMUND 3 Juventus 1 1997
Hernán CRESPO AC MILAN 3 Liverpool FC 3 2005
Filippo INZAGHI AC MILAN 2 Liverpool FC 1 2007
Diego MILITO INTE MILAN 2 FC Bayern München 0 2010
Karlheinz RIEDLE BV BORUSSIA DORTMUND 3 Juventus 1 1997
Hernán CRESPO AC MILAN 3 Liverpool FC 3 2005
Filippo INZAGHI AC MILAN 2 Liverpool FC 1 2007
Diego MILITO INTE MILAN 2 FC Bayern München 0 2010
MCHEZAJI KUFUNGA FAINALI MBILI TOFAUTI
RAÚL González (Real Madrid CF) 2000 [Bao 1l], 2002 [Bao 1]
Samuel ETO’O (FC Barcelona) 2006 [Bao 1], 2009 [1]
Lionel MESSI (FC Barcelona) 2009 [1], 2011 [1]
KLABU ZA NCHI MOJA KUCHEZA FAINALI
Real Madrid CF 3 Valencia CF 0 Paris 2000
AC Milan 0 Juventus 0 Manchester 2003
[AC Milan walishinda kwa penati 3-2]
Manchester United FC 1 Chelsea FC 1 Moscow 2008
[Manchester United FC penati 6-5]
VIWANJA VILIVYOWAHI KUCHEZEWA FAINALI
(Mara zake kwenye Mabano)
AMSTERDAM (1) (Amsterdam Arena, 1998)
ATHENS (2) (Olympic Stadium, 1994, 2007)
BARCELONA (1) (Camp Nou, 1999)
GELSENKIRCHEN (1) (Arena AufSchalke, 2004)
GLASGOW (1) (Hampden Park, 2002)
ISTANBUL (1) (Atatürk Olimpiyat Stadi, 2005)
LONDON (1) (New Wembley Stadium, 2011)
MADRID (1) (Estadio Santiago Bernabéu, 2010)
MANCHESTER (1) (Old Trafford, 2003)
MILAN (1) (Stadio Giuseppe Meazza, 2001)
MOSCOW (1) (Luzhniki, 2008)
MUNICH (2) (Olympiastadion, 1993, 1997)
PARIS (2) (Stade de France, 2000, 2006)
ROME (2) (Stadio Olimpico, 1996, 2009)
VIENNA (1) (Ernst-Happel-Stadion, 1995)
WACHEZAJI WALIOKOSA FAINALI KWA KUFUNGIWA
Alessandro COSTACURTA & Franco BARESI (AC Milan) v FC Barcelona 1994
Michael REIZIGER (AFC Ajax) v Juventus 1996
Roy KEANE & Paul SCHOLES (Manchester United FC) v FC Bayern München 1999
Amedeo CARBONI (Valencia CF) v Real Madrid CF 2000
ZE ROBERTO (Bayer Leverkusen) v Real Madrid CF 2002
Pavel NEDVED (Juventus) v AC Milan 2003
Eric ABIDAL & DANIEL ALVES (FC Barcelona) v Manchester United FC 2009
Darren FLETCHER (Manchester United FC) v FC Barcelona 2009
Franck RIBÉRY (FC Bayern München) v FC Internazionale Milano 2010
THIAGO MOTTA (FC Internazionale Milano) v FC Bayern München 2010
José PINTO (FC Barcelona) v Manchester United FC 2011
KADI NYEKUNDU KWENYE FAINALI
Jens LEHMANN ARSENAL FC v FC Barcelona [Mwaka 2006 Dakika ya 18]
Didier DROGBA CHELSEA FC v Manchester United FC [2008 Dak ya 116]
KLABU ZILIZOWAHI KUCHEZA FAINALI
Mara 6
AC Milan (1993, 1994, 1995, 2003, 2005, 2007)
Mara 4
FC Barcelona (1994, 2006, 2009, 2011), Juventus (1996, 1997, 1998, 2003), Manchester United FC (1999, 2008, 2009, 2011)
Mara 3
Real Madrid CF (1998, 2000, 2002), FC Bayern München (1999, 2001, 2010)
Mara 2
AFC Ajax (1995, 1996), Valencia CF (2000, 2001), Liverpool FC (2005, 2007)
Mara 1
Olympique de Marseille (1993), BV Borussia Dortmund (1997), Bayer 04 Leverkusen (2002), FC Porto (2004), AS Monaco FC (2004), Arsenal FC (2006), Chelsea FC (2008), FC Internazionale Milano (2010)
WASHINDI WA UEFA CHAMPIONZ LIGI
MATAJI MATATU
AC Milan (1994, 2003, 2007), Real Madrid CF (1998, 2000, 2002), FC Barcelona (2006, 2009, 2011)
MATAJI MAWILI
Manchester United FC (1999, 2008)
TAJI MOJA
Olympique de Marseille (1993), AFC Ajax (1995), Juventus (1996), BV Borussia Dortmund (1997), FC Bayern München (2001), FC Porto (2004), Liverpool FC (2005), FC Internazionale Milano (2010)
NCHI AMBAZO KLABU ZAKE ZIMETWAA UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mataji 6
SPAIN (1998, 2000, 2002, 2006, 2009, 2011)
Mataji 5
ITALY (1994, 1996, 2003, 2007, 2010)
Mataji 3
ENGLAND (1999, 2005, 2008)
Mataji 2:
GERMANY (1997, 2001)
Taji 1
FRANCE (1993), NETHERLANDS (1995), PORTUGAL (2004)
...endelea kuperuzi zaidi na BUKOBASPORTS upate habari zaidi za ki-sports
No comments:
Post a Comment