BUKOBA SPORTS

Friday, May 4, 2012

VPL: AZAM V MTIBWA KURUDIANA LEO, SIMBA NA YANGA JUMAPILI

Kufuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kuamuru Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL, kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar irudiwe leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuatia Rufaa ya Timu ya African Lyon, Mechi za mwisho za Ligi zilizokuwa zichezwe Jumamosi sasa zitachezwa Jumapili pamoja na ile BIGI MECHI kati ya Simba na Yanga.
 African Lyon ilikata Rufaa ikitaka Mtibwa Sugar ishushwe Daraja kwa kugomea Penati walipocheza na Azam Uwanja wa Chamazi huku gemu ikiwa 1-1 na hali hiyo ilisababisha Mechi hiyo ivunjike Dakika za mwishoni.

Akizungumza na Wanahabari hapo jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema Kikao cha Kamati ya Nidhamu kilichoketi juzi kusikiliza Rufaa ya African Lyon na kilitupilia mbali maombi hayo kwa kuwa Mtibwa Sugar haikuvunja mechi na badala yake Refa aliechezesha mechi hiyo ndiye alivunja mchezo huo kabla ya kusubiri muda wa kisheria wa Dakika 15 tangu pambano lisimame na ndio avunje Mechi.
Hivyo, Osiah alisema kuwa Kamati ya Nidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Ligi hiyo iliamuru mechi hiyo kurudiwa kwani ni Refa ndie alievunja pambano na wala sio Mtibwa Sugar kama ilivyoelezwa kwenye Rufaa ya African Lyon.
Awali Kamati ya Ligi iliamuru kuipa Azam Pointi tatu na Mabao 3.
Klabu ya Azam imethibitisha kucheza Mechi ya leo na ikiwa itatoka sare au kufungwa basi moja kwa moja Bingwa ni Simba.

MSIMAMO WA TIMU ZA JUU VPL
[Kila Timu imebakisha Mechi 1 isopkuwa Azam bado 2]
1 Simba Mechi 25 Pointi 59==Tofauti ya Magoli 30
2 Azam Mechi 24 Pointi 53==Tofauti ya Magoli 25
3 Yanga Mechi 25 Pointi 49

RATIBA:
Jumapili Mei 6 MECHI ZA MWISHO za LIGI
Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa)
Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha)
Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi)
Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga)
African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro)
Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam)
Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).

No comments:

Post a Comment