Mchezaji RVP anaweza akawa njiani kuondoka kunako klabu ya Arsenal baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.
Taarifa toka katika website yake ilisema ya kuwa mchezaji huyo hana mpango wa kuongeza mkataba klabuni hapo.
Taarifa hiyo inawafanya Man City kujiweka sawa na kujiandaa ili kuweza kumpata mchezaji huyo kwani wamekuwa wakimfuatilia kwa mda mrefu sasa.
“Hili ni Tangazo kwa mashabiki wangu kuhusiana na uamuzi wangu.
Nimekaa kimya mda wote huu kwa heshima na uzalendo nliokuwa nao kwa klabu na kama tulivyokubaliana na Mr Gazidis na Mr Wenger. Lakini kutokana na habari nyingi zinazoskika katika vyombo vya habari, nadhani ni bora na nyie mashabiki mjue ni nini kinaendelea.
Kama ilivyokuwa imetangazwa mwanzoni nlikuwa na kikao na Bosi na Gazidis. Kikao kilihusu mustakabali wa klabu na falsafa yao. Ila swala la mkataba halikuzungumziwa.
Kwa upande wangu nlikuwa na msimu mzuri sana lakini lengo langu kubwa ni kushinda vikombe na kuirudisha timu katika mafanikio.
Kutokana na heshima kubwa nliyokuwa nayo kwa Mr Wenger, wachezaji wenzangu na mashabiki sitaki kutoa maelezo zaidi ila kwa kifupi ni kuwa katika mkutano huo ilikuwa wazi mambo waliyokuwa yakiongelewa kuhusu jinsi ya kuiendesha timu ni tofauti na muono wangu nliokuwa nao na hivyo sikukubaliana nao.
Nimefikiria kwa umakini sana na kwa muda mrefu sana na kuamua kutosaini mkataba mpya. Najua mashabiki mtapinga swala hili la mie kukataa kusaini mkataba na naheshimu na kuelewa ni kwanini mtakataa.
Naipenda klabu hii na mashabiki wake. Nimekulia hapahapa Arsenal.
Kila mtu katika klabu hii wamekuwa wakinisaidia daima miaka yote hii na nimekuwa nkijitahidi kurudisha fadhila uwanjani na nje ya uwanja. Ninafuraha sana ya kuwa sehemu ya klabu hii kwa mda wote huu wa miaka minane.
Pindi Mr Gazidis atakaporudi toka likizo yake ya Amerika tutaongea zaidi na baada ya hapo ntawataarifu yatakayokuwa yanaendelea”.
No comments:
Post a Comment